MVUA KUBWA INAYOAMBATANA NA PEPO,NGURUMO KALI INAENDELEA KUNYESHA MTWARA

Majira ya saa  mbili kasorobo (1:45) asubuhi hii ya jumanne  31/1/2017 eneo la  mtwara Mjini manispaa ya mtwara mikindani mkoani mtwara mvua kubwa inayoambatana na ngurumo,radi na pepo kali  inayesha na kusababisha usumbufu kwa wakazi wa eneo hilo  has a wanafunzi na wafanyabiashara wa Mjini hapa.
Zaidi ni ujenzi wa uboreshaji wa miundombinu ya barabara nyingi za hapa Mjini pamoja na ujenzi wa mifereji au mitalo ya kupitisha maji ya mvua kuwa bado mingi haijakamilika hivyo kuhofiwa kwa kuondolewa kwa vifusi na dhana za ujenzi ambazo ziko maeneo ya ujenzi.
Pia kuna hofu ya kuweza kutokea mlundikano wa maji ktk mitalo hiyo na hats makazi ya watu endapo mvua hiyo itaendelea kunyesha kwa kasi hiyo.
Kumekuwa na kukosekana na kususuasua kwa unyeshaji wa mvua mkoani mtwara ambapo zilitarajiwa kuanza toka mwezi desemba.





Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MVUA KUBWA INAYOAMBATANA NA PEPO,NGURUMO KALI INAENDELEA KUNYESHA MTWARA"

Back To Top