JOTO UCHAGUZI MKUU LAPANDA KENYA NA RWANDA

Hekaheka za joto la uchaguzi mkuu  ktk mataifa mawili ya africa mashariki laanza kupanda,nchi hizo ni kenya na rwanda,imekuwa ni kawaida ya nchi ya kenya kila unapokaribia uchaguzi mkuu kutokea kwa fujo na maandamano kama ilivyoshuhudiwa mwishoni mwaka jana huko jijini nairobi ktk ofisi ya tume ya uchaguzi wa kenya IEBC ktk kushinikiza kujiuzulu kwa uongozi huo na kuchaguliwa tena ulio huru.
Kenya ni nchi inayotafunwa sana na swala la ubaguzi wa kikabila,ugaidi ktk mipaka yake na somalia,westgate mall,chuo cha garissa,na vurugu za kidini mkoa wa pwani mjini mombasa.
Muunganano wa vyama vya upinzani cord umesisitiza kuufanya uchaguzi huo kuwa huru na haki na si vyenginevyo.
Lakini nchini rwanda kwa bwana paul kagame napo ali si shwari sana kwani nao wanajitaarisha na swala hilohilo la uchaguzi,rwanda pia ni taifa lenye kusumbuliwa na ukabila hasa baina ya wahutu na watutsi ambao mnamo mwaka 1994 ulipelekea mauaji ya kimbari na kusababisha mgawanyiko wa kimatabaka.Rwanda inatarajiwa kufanya uchaguzi mkuu 4/8/2017.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "JOTO UCHAGUZI MKUU LAPANDA KENYA NA RWANDA"

Back To Top