Ubongo wa mwanadamu huendelea kuwa na Afya njema hadi kufika umri wa miaka 20 baada hapo huanza kupoteza uwezo wake wa utendaji kazi,lakini pia tusisahau kuwa ngozi ya mwanadamu hujibadili muonekano wake kila baada siku 28 tu,miongoni mwa mambo yanayoweza kumfanya mtu kuzeeka kwa haraka ni kutokana na uasilia wake wa kikoo!! (Genetic heredity biological makeup from his parents or generation) utakubaliana kuna baadhi ya watu huanza kuwa na mvi,uaraza mapema sana!! Hiyo hutokana na uasilia na haepukiki kamwe!! Yafuatayo ni mambo ya kufanya au kuepuka ili kuukimbia uzee wa mapema:- Kuepuka kukaa au kufanya kazi kwa muda mrefu ktk jua Kali sana,kuacha uvutaji wa sigara na vinavyofanana na hivyo,kufanya kazi zinazotumia nguvu kupita uwezo Mara wa Mara,kuepuka misongo ya mawazo ya mda mrefu,(stress and depression),unywaji wa pombe na vileo vya aina zote,kupata muda mwingi a kupumzisha mwili hasa kulala,kula vyakula vyenye protein,wanga,vitamini ktk Milo ya kila siku,kuepuka kufanya ngono Mara nyingi mfululizo,kunywa maji ya kutosha,mazoezi,kwa wanawake kuzaa kwa mapngilio na sio uzazi wa papo kwa papo bila kupumzika kwa muda usiopungu miaka mitatu!!! Hii itatusaidia kupunguza uzee wa haraka usioendana na umri!!


0 Comments "JINSI YA KUEPUKA KUZEEKA HARAKA"