
Majibu ya mitihani hiyo yalionekana mabaya kabisa kwa upande wa walimu baada ya kusahihishwa,hali hii ilimsitua gavana wa jimbo hilo la Kaduna Ndugu Nasri-el Rufai na kutoa maamuzi magumu ya kutaka kuwafukuza kazi walimu wote waliofanya jaribio hilo na kufeli.
Gavana Rufai amenukuliwa akisema kuwa kwa sasa wako mbioni kuajili walimu wapya wenye vigezo na uwezo zaidi na kuwaondoa wale wote waliofanya vibaya.

Makundi kama Boko Haram ndio makundi yanayosumbua kaskazini na nchi nzima ya nigeria kwa kufanya mashambulizi ya kujitolea mhanga,shule nyingi za msingi na sekondari zimeharibiwa vibaya au kuchomwa moto na vikundi hivi na kusababisha kufungwa kwa shule hizo hadi sasa na zaidi ya wasichana 300 walitekwa nyara na kikundi hiko na wengi wao hawajapaikana hadi leo.
Kiwango cha elimu kwa nigeria kaskazini kimekuwa cha chini zaidi ukilinganisha na kusini mwa nchi hiyo,hali hii imefanya walimu wengi kuacha au kukimbia kazi ktk maeneo hayo kwa kuhofia usalama wa maisha yao.
0 Comments "WALIMU 21,780 WALIOFELI MITIHANI SHULE ZA MSINGI KUTIMULIWA KAZI"