TRUMP KUWAUMBUA WALIOPANGA NA KUMUUA JF KENNEDY 1963

Rais Donald Trump amenukuliwa na vyombo vya habari jana jumamosi kuwa yuko tayari kutoa ruhusa ili kutoa ushahidi,mipango na mauaji ya aliyekuwa rais wa marekani aliyeuawa  akiwa ktk kampeni ktk kuwania kipindi cha pili cha madaraka yake ktk jiji la Dallas jimbo la Texas,kennedy aliuawa kwa kupigwa risasi kadhaa maeneo ya kifuani na tumboni na mtu aliyefahamika kwa jina la Lee Harvey Oswald siku ya Novemba 22 1963 majira ya saa 12:30 mchana akiwa amebebwa ktk gari maaalum ya wazi na familia yake.

Zaidi ya watu wawili waliuawa na wawili wengine kuumia vibaya eneo la tukio ktk nje ya jengo la Dealley plaza,Kennedy aliuawa mda mchache tu baada ya kushuka ktk uwanja wa ndege wa Dallas,Rais Trump amelishikia kidete swala hili la mauaji ya Kennedy na kusema yuko tayari kutoa ruhusa kwa maafisa wa shirika la ujasusi la marekani CIA na shirika la upelelezi FBI kutoa ukweli mzima wa mauaji ya JF kennedy kwa wananchi wa marekani ifikapo Oktoba 26 kwa kuliataka baraza la Congress kupitisha ombi hilo.

Taarifa za kifo cha JF Kennedy rais wa 35 wa marekani zimeendelea kuwa siri kubwa kwa vyombo vya usalama kwa utatanishi wake na hata kuusishwa kwa baadhi wa maafisa wa ngazi za juu wa serikali ktk mauaji hayo.



Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "TRUMP KUWAUMBUA WALIOPANGA NA KUMUUA JF KENNEDY 1963"

Back To Top