KING'UNGE MUGABE KUZULU AFRIKA KUSINI BILA MKEWE

Mtawala mkongwe zaidi Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe yuko nchini afrika kusini kwa ajili ya kumtembelea mwenyeji wake Jacob Zuma kuzungumzia maswala mbalimbali yahusiayo na uchumi wa nchi zao hizo mbili,Mugabe amekuwa akiitembelea Afrika ya kusini mara kwa mara ili kuimarisha mahusiano yake na jirani yake huyo.

Mugabe amewekewa vikwazo kadhaa na jumuiya za umoja wa ulaya (EU),marekani na nchi nyingi za ulaya kwa kile kinachoonekana kukiuka haki za kibinadamu ktk nchi yake ya zimbabwe hasa kwa kukandamiza vyama vya upinzani.

Mugabe mwenye umri wa miaka 93 kwasasa ndio rais mwenye umri mkubwa zaidi brani afrika,ameiongoza zimbabwe toka mwaka 1980 ilipopata uhuru toka kwa waingereza,ametembelea afrika kusini kwa ajili ya kuweka uhusiano wa karibu na nchi hiyo na kuweka sawa baadhi ya mikataba ya kiuchumi ambayo ilishakuwepo kwa mda mrefu.

Mugabe ameapa kuingoza zimbabwe mpaka pale kifo kitakapomfika,hali hii imemfanya kuonekana kuonekana kuwa dikteta kwa mataifa ya nje.

Safari hii Mugabe amezulu afrika kusini bila kuambatana na mkewe Grace Mugabe na kuwafanya waafrika kusini kuhisi sababu kuu ya kutokuja kwa mkewe ni kutokana na kisa alichokifanya moja ya safari yake nchini humo kwa kumpiga msichana wa kiafrika kusini na kumuumiza sehemu ya paji la uso.



Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "KING'UNGE MUGABE KUZULU AFRIKA KUSINI BILA MKEWE"

Back To Top