KENYA YAANDIKA HISTORIA KWA KURUDIA UCHAGUZI UPYA

Kenya imekuwa nchi ya ajabu na ya kwanza duniani kwa kufuta uchaguzi na kurudia upya baada ya kuwepo kwa malalamiko ya pende wa upinzani wa NASA unaogoonzwa na Kiongozi Raila Odinga kwa kupeleka malalamiko mahakama kuuu ya kenya kwa ajili ya kutaka uchaguzi huo urudiwe kutokana na makosa mengi yaliyojitokeza ktk shughuli nzima hiyo.

Uchaguzi huo ambao ulifanyika siku ya jumanne agosti 8 2017 ulizua utata pale yalipotangazwa matokeo kuwa Uhuru kenyatta ndio Mgombea aliyechaguliwa na wakenya kuwa rais wao kwa kipindi hiki cha pili.

Raila odinga na kambi yake ya upinzani ya NASA walipeleka ripoti yenye nakala elfu 20 kunyesha udhaifu na ubabaishaji mwingi uliojitokeza ktk uchaguzi huo na kufanya wapinzani nwengi kushindwa kuapata haki zao za kuchaguliwa na wananchi.

Kufuatia sakata hilo mahakama kuu ya kenya iliamua kusikiliza malalamiko hayo na kuamua kuyafanyia kazi na hatimaye  siku ya ijumaa 1 septemba majaji sita akiongozwa na jaji mkuu wa kenya David Muraga alitangaza kurudiwa upya kwa uchaguzi wa kenya ndani ya siku 60 zijazo.

Rais Uhuru Kenyatta alionyesha kusikitishwa na maamuzi hayo na kusema yeye bianafsi hayakubali maamuzi hayo lakini anayaheshimu na atatekeleza kama mahakama ilivyoamua.

Kambi ya NASA na wafuasi wake wamefurahishwa sana na maamuzi hayo na kufanya maelfu ya wanachama wa chama hiko kumiminika barabarani huku wakishangilia kuwa sasa mahakama imeonyesha kufanya kazi na kutenda haki kwa wananchi kwa kiasi kikubwa hivyo kuvunja rekodi ya dunia kwa Kenya kufanya maamuzi magumu naya nadra sana kuwahi kutokea ktk dunia.




 chini kabisa ni timu ya majaji watano wa mahakama kuu ya kenya wakiongozwa na jaji mkuu David Muraga waliofanya maamuzi ya kutengua kwa uchaguzi mkuu wa kenya na kufanya urudiwe tena ndani ya siku 60 zijazo,wanne walipiga kura ya uchaguzi urudiwe na wawili walitaka usirudiwe.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "KENYA YAANDIKA HISTORIA KWA KURUDIA UCHAGUZI UPYA"

Back To Top