ISRAEL,IRAN VITANI

Ushahidi wa picha za satalaiti za israel zimoenyesha kuwa Iran bado inaendelea na mikakati yake ya kutengeneza silaha zal kisasa kabisa za kinyuklia ndani ya taifa la syria baada ya kuona mataifa ya kigeni yamegundua mbinu zake za kurutubisha madini ya uranium ndani sasa wameamua kuhamisha kiwanda hiko ktk taifa la jirani la syria ili kukwepa kuonekana na mataifa mengine.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyau ameliambia baraza la usalama la UN kuwa ikiwa iran itaaachiwa kufanya hivyo basi wajue wazi kuwa taifa la israel na dunia kwa ujumla itakuwa ktk hatari ya kuharibiwa na silaha hizo.

Netanyau amesema kuwa iran ilishaapa kulifuta taifa la israel ktk uso wa dunia kwa njia yeyote ile ikiwemo hata ya vita,iran,syria ni miongoni mwa mataifa machache yanayopinga kuwepo kwa taifa la israel toka kuanzishwa kwake miaka ya 1967.

Urusi kwa upande wake wanapinga uvumi huo wa kuwa iran inaendelea kurutubisha madini ya kinyuklia kwa ajili ya kutengeneza silaha za kisasa zaidi ndani ya syria.

Makundi kama Hizbollah la lebanon,Hamas la Gaza ni miongoni mwa makundi yanayoifanya israel ishindwe kupata usingizi,hta hivyo israel imeapa kuivamia iran ikiwa usalama wake utakuwa mashakani zaidi.







Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "ISRAEL,IRAN VITANI"

Back To Top