Matokeo ya uchaguzi wa kenya uliofanyika siku ya jumanne tarehe 8 mwezi agosti 2017 yametangazwa rasmi jana ktk ukumbi maalum wa Bomas jijini Nairobi.
Tume rasmi inayohusika na kuandaa,kusimamia uchaguzi na kutangaza matokeo ya chaguzi za nchi hiyo ya IEBC imemtangaza Uhuru kenyatta kuwa ndio mshindi wa uchaguzi huo kwa kumshinda mpinzani wake Raila odinga kwa asilimia 54.3% na kumuacha Raila odinga kwa kupata 44.7% hivyo kuleta fujo mitaani mda mchache tu baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo kwa wapinzani kushindwa kukubaliana na taarifa hizo za wao kushindwa ktk kiti cha uraisi.
Watu kadhaa wamejaruhiwa na na wawili kuripotiwa kufa kwa kupingwa na polisi wakiwa ktk hali ya kuthibithi usalama na amani ya miji mbalimbali iliykubwa na machafuko hayo.
Raila odinga amekuwa akilalamika kuwa tume ya uchaguzi ya IEBC haikuwa huru na ya haki ktk kusimamia mchakato mzima wa kuandaa,kusimamia na kutangaza matokeo ya uchaguzi huo hivyo kukumbwa na sintofahamu kubwa kwa wananchi kutokupata baadhi ya matokeo ya majimbo.
Hata hivyo mda mchache tu baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi huo Mh.Uhuru kenyatta ametoa hotuba nzuri na kunganisha taifa kwa kusema "Wao wote ni waoja na uchaguzi umeshakwisha sasa wanatakiwa kuwa kitu kimoja kwa
kuunganika na kuleta tija za kimaendeleo ktk nchi zao bila kujali maslahi ya vyama vya kisiasa,yeye binafsi atakaa nao chini wapinzani wote na kufanya nao mazungumzo juu ya kulipeleka taifa mbele zaidi"
0 Comments "UHURU KENYATTA ABEBA TENA KITI CHA UHURU CHA KENYA "