
Ndege hizo ambazo ilikuwa ni ahadi ya rais John Pombe Magufuli ikiwa ni awamu ya pili baada ya zile mbili za Q400 Bomberdier kuingia mwaka jana na kuahidi kuingia nyingine mwaka huu ifikapo mwezi julai,Ndege hizo zote nne zilikuwa zimeshalipiwa pesa taslimu isipokuwa kwa hizo mbili zitazotoka ktk kampuni ya Boeing ya marekani ambazo zitakuwa na uwezo wa kwenda mbali zaidi bila kuwa na vituo mara kwa mara kwa ajili ya kuongeza mafuta aukupumzisha injini.

Tundu lissu amesema kilichosababisha ndege hizo kushindwa kuingia nchini kwa mwezi julai kama ilivyotarajiwa ni baada ya kampuni ya kikanada kuzishikilia ndege hizo kwa madai ya mabillioni ya shilingi ikiwa kama tozo lililotolewa na mahakama kwa mwaka 2010 baada ya serikali kusitisha mkataba wa ujenzi wa barabara ya Wazohill -Bagamoyo kwa kisa cha kukiuka mkataba ktk ujenzi wa barabara hiyo wakati Magufuli akiwa ndio waziri wa miundombinu.

Kampuni hiyo iliamua kwenda mahakamani na kuishitaki serikali na kuamuliwa kuilipa shilingi bilionin 50 kwa mwaka 2010 lakini serikali ilikataa na kukaa kimya hivyo kufanya riba kupanda kwa miaka saba mfululizo na kufikia zaidi ya bilioni 80.
Kwa habari kamili tazama video hii hapa chini.......
0 Comments "TUNDU LISSU AANIKA HADHARANI JUU YA NDEGE ZA BOMBERDIER KUSHINDWA KUFIKA NCHINI "