MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI VENEZUELA AKIMBILIA COLOMBIA

Aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali nchini venezeule mwanamama Luisa Ortega Diaz  ameikimbia nchi yake baada wiki chache tu baada ya kufukuzwa kazi na mahakama ku ya venezuela kwa kuonekana kwenda kinyume na maadili yakazi yake kwa kukiuka amri za Nicolas Maduro aliyeshika madaraka kutoka kwa mwanaujamaa Hugo Chaves aliyefariki.
Mwanasheria huyo aliyekimbilia nchi ya jirani ya Colombia kwa kupitia njia ya majini kutumia boti iendayo kasi kubwa aliingia ktk mji wa Aruba akiwa na ndege binafsi baada ya boti hiyo kumfikisha mahali fulani na kundelea na usafiri wa anga.

Mwanasheria huyo kwa sasa yuko ktk mji mkuu wa Colombia wa Bogota,amesema sababu iliyomfanya kukimbia nchi yake ni kuhofia usalama wa maisha yake baada ya kufukuzwa kazi na Mahakama kuu ya nchi yake.
Serikali ya Venezuela inayoongozwa na Rais Nicolas Maduro imekuwa ikilaumiwa na mataifa ya nnje kwa kukandamiza hali ya kidemokrasia na kuua waandamanaji wanaoingia mitaani kwa kupinga kubadilishwa kwa katiba ili kuongeza kipindi cha utawala.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI VENEZUELA AKIMBILIA COLOMBIA"

Back To Top