MAREKANI,UMOJA MATAIFA WAHAHA KUIZIBITI KOREA KASKAZINI KWA VIKWAZO

Marekani na umoja wa mataifa wamekuwa ktk vikao mara kwa mara ndani ya wiki hii ili kuangalia na kuapanga kwa hatua za kuichukulia nchi ya korea kaskazini kuhusiana na harakati zake za kuendelaea na kurusha makombora ya masafa marefu kwa majiani zake wa korea kusini na japani.
Mara kwa mara marekani,umoja wa ulaya na umoja wa mataifa wamekuwa wakiiwekea vikwazo vya kiuchumi nchi hii ya korea kaskazini kutokana na halin yake ya uchokozi kwa majirani zake hao.

Korea kaskazini kwa zaidi ya miongo saba sasa imekuwa mbioni ktk harakati zake za kuendelea kuzitafurta silaha za kinyuklia zenye nguvu  na uwezo wa kufika hadi taifa la marekani hasa ktk mji mkuu wa Washinghton ambao uko zaidi ya kilomita elfu kumi kutoka mji mkuu wa Pyongyamg nchini korea kusini.
Toka kuingia kwa uongozi wa Kija Kim Jong Un ambaye amerithi utawala huo kwa baba yake mzazi Kim Jong Il baada ya kufariki,kumekuwa na majaribio ya mara kwa mara ya makombora ya masafa maefu ambayo uelekezwa nchi za Korea kusini na Japan,hali hii inazidi na kuwatia hofu hata mataifa ya ulaya na mrekani na kuwalazimisha kuingilia mgogoro huo kwa kuendelea kuionya kwa kuiwekea vikwazo vya kiuchumi korea kaskazini mara kwa mara.

Baadhi ya vikwazo hivyo ni kukataa kununua kwa makaa ya mawe,malighafi za chuma,samaki kutoka nchini humo,washirika na wanunuzi wakubwa wa bidhaa kutoka korea kaskazini ni China,urusi,cuba ambao nao wanajitahidi kuweka vikwazo kwa kadri ya uwezo wao bila mafanikio ya aina yeyote na kuifanya iendelee kufanya majaribio zaidimkila baada ya mda mfupi sana,

Korea kaskazini imekuwa ikijitete inafanya hivyo kwa kujiweka tayari na adui yeyote atakaye jaribu kuitishia au kuivamia nchi yao hiyo.

Umoja wa mataifa,marekani,china na urusi zimekutana ili kuangalia njia za kiuchumi ambazo wanaweza kuichukulia na kuibana korea kaskazini ili kusitisha mipango yake hiyo ya silaha za kinyuklia ianayokwenda kwa kasi kila kukicha.



Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MAREKANI,UMOJA MATAIFA WAHAHA KUIZIBITI KOREA KASKAZINI KWA VIKWAZO"

Back To Top