Vipo vifaa vingi sana vinavyotumika kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kijeshi,utafiti ikiwemo meli,monowari na nyambizi,Mashine hii inayoweza kuwa ng'eni masikioni a machoni mwako ni miongoni mwa viffaa vya kisasa kabisa vinavyotumika na wanajeshi au wanasayansi ktk shughuli zao hizo za kijeshi au utafiti ktk mazingira ya chini ya maji mengi kama ziwani na baharini ambapo mtu hawezi kufika ila kwa msaada wa vifaa maalum kabisa kama hichi vcha nyambizi.
Nyambizi zilianza kutumika rasmi ktk vita ya kwanza ya dunia iliyopiganwa mnamo miaka ya 1939-1945 baina ya mataifa ya ulaya yenye nguvu yakiwemo italia,ujerumani,japan,austria,hungary,uingereza.
Mbio hizi za kugundua na kutengeneza mashine hii zilikuja baada ya kuona vita za baharini zinakuwa ngumu sana hasa inapokuwainapiganwa juu au chini ya maji.,kwakuwa vita ya ardhini inahitaji magari,vifaru,bunuki,vita ya anga inahitaji hasa ndege zitakazobeba silaha nzito ili kumshambulia adui swli likabaki je vita ya baharini au ktk maji itahitaji nini? Jibu likawa itahitaji kifaa maalum kitachoweza kuwepo chini ya maji kuona na kushambulia maadui hata kama watapita kwa njia hiyo ya chini ya maji.
Usalama wa mataifa mengi yaliyoendelea yanajilinda sana kupitia njia za chini ya maji na sio juu,ardhini au angani pekee.
Mataifa kama marekani,japan,italia,ujerumani,urusi,uingereza na mengine mengi yliyo juu kijeshi hasa yale ya barani ulaya yatengeneza na kumiliki aina hii ya mashine za kisayansi na kijeshi,nyambizi ni kifaa cha gharama kubwa na kinahitaji ujuzi wa hali ya juu sana kuanzia kutengenezwa kwake na hata ktk kumiliki.
Nyambizi hadi sasa ziko za aina mbili tu yaani zile zinazotumia nishati ya mafuta ya diesel na zile zituazo nishati za kisasa kabisa ya Nyuklia.,nyambizi ugharimu kuanzia dola milioni 400 hadi bilioni 4.5 kwa nyambizi moja tu,ina maumbile ya samaki nyangumi au papa na huwa na uzito wa tani hadi 6,000.
Nyambizi moja inaweza kuchukua watu wa kawaida au wanajeshi kuanzia 2 hadi 100 kwa wakati mmoja tu,ina mwendo kasi wa knot 12 hadi 40 kwa maili 46 kwa saa moja.
Ina uwezo wa kuzama na kuibuka ndani ya maji baada ya kujazwa au kutolewa kwa maji au hewa kwenye mtungi wake maalum.
Nyambizi ina uwezo wa kukaa chini ya maji ikiwa na watu bila kuibuka kwa mda wa miezi 3 hadi 6 bila kuibuka juu ya maji kutegemeana na chakula kinaweza kutosha walioko ndani kwa mda wote huo,nyambizi hizi hasa ni zile zinazotumia nishati za kinyuklia ambazo ina uwezo wa kukaa kwa miaka ipatayo 30 bila kuongezwa nishati nyingine ukitofautisha na zile za diesel ambazo nhukaa kwa masaa 38 tu na kuibuka tena ili kuongeza nishati upya.
Titanium na alloyed steel metal ndio aina ya vyuma imara kabisa zisizo chakaa au kutoka kutu kwa haraka hata zinapokutana na maji ya chumvi kali kama ya bahari,nyambizi ina uwezo wa kuzama ktk maji kwa kina cha hadi futi 2,400 au mita 730 hii ikiwa ni changamoto ktk sehemu zenye kina kirefu zaii kama kule MARIANA TRENCH iliyopo kule bahari ya pasifiki karibuni na kisiwa cha GUAM .
Kazi kubwa ya mashine au kifaa hiki cha kivita ni kulinda mazingira ya usalama wa majini kwa kuogopa kusambuliwa au kuingiliwa na maadui kwa kupitia njia hizo zisizo rasmi.
Nyambizi ubeba mabomu mengi yaliyo na uwezo wa kushambulia adui aliye ndani ya maji au angani kwani mashine hii imetengenezwa kwa teknologia ya hali ya juu sana inayotumia mifumo ya kisasa ya kompyuta,satelaiti kujua na kuona adui alipo na kushambulia.
Ni nchi chache sana hadi sasa duniani zenye kuwa na uwezo wa kumiliki aina hii ya mashine ya kijeshin na kisayansi ili kujilinda na maadui wa majini.
Baadhi ya nyambizi maarufu duniani ni kama TRIDENT,RUSSIA AKULA,CHINESE KILO,USS LOS ANGELES,HMS VANGUARD,YESEN,OSCAR na nyinginezo nyingi zinazomilikiwa na mataifa yaliyoendelea kiteknolojia.
Korea kaskazini wao pke yao wana nyambizi zipatazo 70,marekani 72,Urusi 24,china,india pia wanamiliki nyambizi nyingi sana za kivita.
0 Comments "MAKUBWA USIYOJUA KUHUSU NYAMBIZI (SUBMARINES)"