BASI YAGONGA TRENI WATATU WAFARIKI

Ajali iliyohusisha basi aina ya coaster na treni imetokea leo alfajiri eneo la kiberege tanesco ktk mkoa wa morogoro manispaa,ajali hiyo ilisababishwa na baada ya basi hiyo kushindwa kuvuka eneo la makutano ya njia ya reli na barabara,basi hiyo ya abiria ilikuwa imepakia wanafunzi na raia wa kawaida ilifeli kuvuka na kufanya treni kuiburuza umbali wa mita 30.

Wanafunzi watatu wamepoteza uhai papo hapo na watu kadhaa kujeruhiwa,wanafunzi hao ambao wametambulika kuwa wanasoma shule ya sekondari ya Kayenzi iliyopo  ktk manispaa hiyo.




Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "BASI YAGONGA TRENI WATATU WAFARIKI"

Back To Top