UJENZI WA BARABARA YA MTWARA,TANDAHIMBA,NEWALA WAPAMBA MOTO

Ile ahadi ya mda mrefu ambayo ilikuwa ndoto kwa awamu zote toka uhuru wa nchi hii utangazwe 9/12/2017 kwa kutengenezwa  kwa barabara ya kutoka mtwara mjini,vijijini,tandahimba hadi newala sasa umeenza kutekelezwa  awamu hii ya tano.

Awamu zote nnen zilizopita zilikuwa zikiahidi kuitengeneza barabara hii kwa kiwango cha lami kutoka mtwara mjini hadi mji wa newala mabapo kuna urefu wa kilomita 104 ila ilikuwa ndoto isiyotimia licha ya kuahidi ktk kampeni za chaguzi zote zilizopita,barabara hii itakwenda kuungana na ile ya masasi na kuwa na urefu wa kilomita 228.

Kuanzia mwezi juni mwanzoni ujenzi wa barabara hii ulianza rasmi kwa ahadi aliyoitoa rais John pombe Magufuli alipoitembelea mtwara mwaka huu mwanzoni.

Ujenzi umeanza kwa awamu ya kwanza za kilomita 50 kutoka mji wa mtwara hadi ktk halamshauri ya Nanyamba iliyopo katikati ya matwara vijijini na Tandahimba.

Barabara hii ambayo ni muhimu kwa kuunganisha wilaya kadhaa ambazo ni muhimu na maarufu kwa kuzalisha zao la korosho ambalo uwapatia wananchi na serikali fedha nyingi kama mapato ina weza kufungua uchumi kwa wilaya hizi ambazo kwa mda mrefu watu wake wamaekuwa wakilalamikia kutokana na ubovu wake hasa nayakati za vipindi vya mvua kubwa,gari nyingi uharibika hivyo kufanya wamiliki wa magari hayo kushindwa kuepeleka magari huko kwa kuhofia kuaharibika na kuapata hasara.





 Picha zikionyesha ujenzi wa barabara ukiendelea ktk hatua mbalimbali eneo la kata ya Naliendele mkoani Mtwara.





Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "UJENZI WA BARABARA YA MTWARA,TANDAHIMBA,NEWALA WAPAMBA MOTO"

Back To Top