UINGEREZA MBIONI KUPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA SIMU ZA MKONONI KWA WATEMBEAJI KWA MIGUU

Baada ya mchi kadhaa duniani kupiga marufuku matumizi ya simu za mkononi kwa waendeshaji wa vyombo vya moto kama magari,pikipiki na aina nyingine za usafiri sasa uingereza imeanza taratibu hatua ktk kuweka sheria kali juu ya watembeaji wa miguu baada ya kuonekana ajali nyingi za barabarani sasa zinasababishwa na watembea kwa miguu wenyewe kwa kutumia vibaya maendeleo ya sayansi na teknologia ya simu za kisasa.

Matumizi makubwa ya simu za aina mbalimbali ktk ulimwengu sasa yameanza kuvuka mipaka kwa kutumika vibaya hata ktk maeneo yasiyo rasmi kama barabarani kutokana na kuja kwa mitandao ya intaneti inayowezesha kutumika ktk whatsapp,facebook,instagram .

Mitandao hii ya aina mbalimbali imewafanya watu kuacha kuwa makini na kutumia mda mwingi zaidi ktk kila eneo ktk kuingia na kufanya mambio mbalimbali  ktk simu zao.

Hali hii imesababisha kuongezeka kwa ajali nyingi barabarani hata kwa watembeaji kwa miguu kujikuta wakigongwa na vyombo vya moto na kuleta maafa makubwa kwa jamii.

Uingereza iko mbioni kwa kutunga sheria itakayowalenga watembea kwa miguu wote ambao watakutwa wakitumia simu wakiwa barabarani huku wanatembea,yeyote atakayekutwa na kadhia hiyo atawajibika kuliapa zaidi ya paundi 100 na kwa yule atatumia simu huku anandesha chombo cha moto atapigwa faini ya paundi 200 pesa za umoja ulaya sawa na laki sita (600,000)



pesa za kitanzania.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "UINGEREZA MBIONI KUPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA SIMU ZA MKONONI KWA WATEMBEAJI KWA MIGUU"

Back To Top