KOREA KASKAZINI YAAPA KUFANYA MAJARIBIO YA MABOMU YA KINYUKLIA HADI KIELEWEKE

Kiongozi wa korea kaskazini Kim Jong Un mwenye kuongoza taifa dogokwa eneo lakini lenye kuogopwa hata na mataifa yenye nguvu za kijeshi dunian kama marekani kwa miongo zaidi ya saba mfululizo baada ya kuendelea kufanya majaribio ya mabomu yake ya kinyulia kwa miaka nenda rudi ili kuhakikisha nia yao ya mabomu hayo siku moja yawe na uwezo wa kufika mji mkuu wa marekani wa Washinghton.

Juzi tu taifa hili limefanya majaribio ya mabomu yake manne na kuyaelekeza pwani ya bahari ya Japan na korea na kusafiri zaidi ya kilomita 3,000 kabla ya kuanguka ktk pwani ya bahari ya japan na kutishia raia wa nchi hiyo.

Korea kaskazini imekuwa na uadui mkubwa na Japan na korea kusini toka vita ya mwaka 1950 ilipoisha baada ya wamarekani kuingilia vita hiyo na kusaidia upande wa washirika wake hao wawili,Korea kaskazini imekusudia kutengeneza injini ya kusafirishia bomu la nyuklia ambayomitakuwa na uwezo wa kuingia ktk miji ya Seoul wa korea kaskazini,Tokyo Japan na ule wa Marekani yaanin washinghton ambao uko zaidi ya kilomita elfu kumi (10,000 km) kutoka mji wa Pyongyang wa korea kaskazini.

Marekani imekuwa ikihaha juu ya atua mbalimbali za kuichukulia nchi hii ikiwemo kuiwekea vikwazo vya kuichumi,kisiasa kwa mda mrefu hata kufikiria kuingilia kijeshi endapo itawezekana,marekani imekuwa ikihofia sana juu ya hatua za kuingilia kijeshi korea kaskazini kutokana na mataifa kama china na urusi ambao wanampa mguvu za kijeshi,kiuchumi na hata kiteknolojia ktk ugunduzi wa silaha za kisasa kila uchao.


Bofya ktk video kutazama tukio zima

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "KOREA KASKAZINI YAAPA KUFANYA MAJARIBIO YA MABOMU YA KINYUKLIA HADI KIELEWEKE"

Back To Top