ALIYEKUWA WAZIRI WA MADINI WILLIAM NGELEJA AREJESHA PESA ZA ESCROW SERIKALINI

Aliyewahi kuwa waziri wa nishati na madini ktk awamu ya tano mh.William Ngelega ameushangaza umma wa watanzania baada ya kuamua kurudisha pesa walizotuhumiwa kukwapua na kugawana kutoka ktk akaunti ya Escrow.

Ktk hali isiyo ya kawaida Mh.william Ngeleja amerudisha zaidi ya shilingi milioni arobaini laki nne na ishirini na tano elfu (40,425,000)




kupitia TRA

Pesa hii ambayo kwa mara ya kwanza ilisemekana kuwa haina wenyewe hivyo baadhi ya viongozi na watu mbalimbali kuamua kuichukua kinyemela na kugawana wao kwa wao kabla ya kugundulika bungeni na kuleta mtafaruku mkubwa kiasi cha baadhi ya viongozi wakubwa toka serikalini kuhusishwa na kashfa hiyo kama Anna Tibaijuka Kuita shilingi milioni 10 kuwa ni pesa ya kununulia mboga tu pale alipokuwa akihojiwa na kamai ya maadili ya umma.

Baada ya kuingia kwa serikali ya utawala wa awamu ya tano inayoongozwa na Mh. John Pombe Magufuli ambayo imekusudia na kuahidi kupambana na ufisadi wa kila aina,tayari imewataja na kuwakamata baadhi ya viongozi waliohusishwa na kashfa mbalimbali nchini.

Baadhi ya viongozi na wafanyabishara walitiwa nguvuni ni mfanyabiashara maarufu na mkubwa wa IPTL Seth na mwenziwe Rugemalila ambaye ndiye mgawaji mkubwa wa fedha hizo kwenda kwa viongozi wa dini na serikali.

Kashfa ya Escrow ilihusisha wizi wa bilioni 320 za kitanzania.




Tazama video hii kuona aliyekuwa waziri wa nishati a madini William Ngeleja akijieleza baada ya kutoka kulipa pesa za escrow TRA.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "ALIYEKUWA WAZIRI WA MADINI WILLIAM NGELEJA AREJESHA PESA ZA ESCROW SERIKALINI"

Back To Top