TRUMP AAMSHA DUDE LA RAUL CASTRO CUBA

Zile jitihada za Rais Barrack Obama za kuweka na kurudisha mahusiano mapya na kisiwa cha cuba walichokuwa n mahusiano nayo mabaya toka 1960 baada ya kufanyika kwa mapinduzi na kiongozi wao Fidel Castro na kuiweka nchi ktk mfumo wa kikomunisti ambao unakinzana na miono ya nchi za magharibi ikiwemo marekani.

Rais Donald Trump yeye amekusudia kwenda kinyume na sera na mabadiliko yote aliayaweka Barrack Obama ikiwemo hili la kuleta maelewano na kisiwa hiki cha kusini mwa marekani kilicho hasimu mkubwa wa marekani,Obama yeye ameamua kujitahidi na kufikia hatua ya kuweka kuwe na mwingiliano wa kiusafiri wa anga na kijamii.

Trum ametangaza sheria mpya na ngumu juu ya mahusiano yake na cuba na hivyo kusababisha tiafa la cuba kutoa taarifa za sheria zao mpya pia kwa kuelekea mahusiano yake na marekani.

Trump ameonekana kuwa kikwanzo kikubwa kwa nchi mahasinmu kama cuba,urusi,korea kaskazini na nchi za mashariki ya kati kwa visngizio vya haki za kibanadamu,ugaidi au kulea magaidi na kusababisha kutangaza vikwazo na sheria ngumu kwa nchi husika kinyume na matawala mwenziwe aliyekuwemo kabla yake aliyeonekana kuwa mwenye kusaka amani zaidi kuliko kusaka matatizo.

Fidel castro alimuachia madaraka mdogo wake Raul castro baada ya hali yake kuwa mbaya kiafya na hatimaye kufariki mwaka 2016 baada ya kuugua kwa mda mrefu.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "TRUMP AAMSHA DUDE LA RAUL CASTRO CUBA"

Back To Top