QATAR YAKATAA MATAKWA 13 YA KUWAIT NA KUSEMA MAMBO YASIYO MASHIKO WALA KUTEKELEZEKA KAMWE

Nchi ya Qatar imekataa wazi matakwa 13 yaliyowekwa na nchi za Yemen,Saudi arabia,Kuwait na nyinginezo ambazo kwa pamoja zimekubaliana kuvunja mahusiano yote na taifa la Qatar kwa kile wanachozania taifa hilo limekuwa likisaidia vikundi vya kigaidi kifedha,silaha na makaz kwa viongozi wake.

Vikundi hivyo ni kama vya al qaeda,Hezbollah,ISIS,kuwa na mahusiano na uturuki,irani,kueneza taarifa za uongo kupitia kituo chao kikubwa cha Al jazeera na kuweka kituo cha kijeshi cha uturuki ndani ya Qatar.

Jana Qatar ilitakiwa kuachana na mambo hayo kukifunga kituo hicho cha matangazo ikiwemo na kulipa fidia kwa mataifa hayo kwa kusababisha hasara kwa kuwekwa kwa vikwazo hivyo.

Leo Qatar imekanusha taarifa hizo na kuziita ni za kijinga na hazina mashiko walaukweli wowote ila ni nia mbaya tu ya majirani zake hao wanatakia nchi hiyo kuwa ktk matatizo,Qatar imesema wao hawawezi kufanyia kazi mambo ambayo hayana maana yeyote ile.

Kuwait ilitoa siku 10 tu kwa Qatar kuyafanyia kazi mambo hayo la vyenginevyo wataiwekea Qatar vikwazo vigumu zaidi ya hivyo.

Taifa hili dogo kabisa la ghuba ya mashariki ya kati ni miongoni mwa mataifa taijri kwa kutegemea rasilimali ya gesi na mafuta inayopatikana hapo kwa wingi.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "QATAR YAKATAA MATAKWA 13 YA KUWAIT NA KUSEMA MAMBO YASIYO MASHIKO WALA KUTEKELEZEKA KAMWE "

Back To Top