QATAR YABANWA MAHALI PABAYA:YAPEWA MASHARTI 13 KUYATIMIZA NDANI YA SIKU 10 ILI KUONDOLEWA VIKWAZO

Wajumbe kutoka Kuwait waipelekea nchi ya Qatar orodha ya masharti 10 kama matakwa kwa nchi zilizokata mahusiano naye wiki mbili zilizopita kwa kuishutumu Doha kuhusika na kusaidia vitendo na makundi ya kigaidi sehemu mbalimbali duniani vinavyofanya mashambulizi yake ndani ya bara arabu na ulaya.

Miongoni mwa masharti ambayo Doha wamepewa kutoka nchi za Misri,yemen,saudi arabia,umoja wa falme za kiarabu, ni kuwa wanaitaka Kufunga kituo chake cha matangazo cha Al-jazeera chenye makao yake makuu ktk nchi hiyo,Kuacha kuwasaidia wanachama wa chama cha Mohamed morsi cha Muslim brotherhood cha misri,kufungwa kwa kituo cha kijeshi cha uturuki kilichopo ndani ya nchi hiyo,kuacha mahusiano na jamuhiri ya kiislam ya Irani.

Kuacha mafungamano na chama caha Hezbollah cha Lebanon,Al qaeda,ISIL au ISIS,qatar pia wamepewa sharti lamkuacha kuwapa uraia watu kutoka nchi nne.

Kwa kutimiza masharti hayo Qatar itaondolewa vikwazo vyote ilivyowelkewa na nchi hizo ikiwa itavitimiza ndani ya siku 10 tu na endapo watakataa kufanya hivyo basi nchi hizo zitachukua hatua ngumu zaidi za kidiplomasia na kiuchumi juu ya nchi ya qatar.

Mpaka sasa qatar bado hawajatoa jibu lolote juu aya masharti na matakwa hayo kutoka kuwait.



Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "QATAR YABANWA MAHALI PABAYA:YAPEWA MASHARTI 13 KUYATIMIZA NDANI YA SIKU 10 ILI KUONDOLEWA VIKWAZO"

Back To Top