HIVI KARIBUNI WATOTO WANATARAJIA KUPORA TAJI LA USHINDI WA MALEZI TOKA VICHWANI MWA WAZAZI (WALEZI) WAO


Inafahamika wazi kuwa ktk kipindi kigumu kabisa ktk malezi ya mtoto baada ya kile cha kubeba mimba (ujauzito) basi kinachofuata ni eneo la ujana kuelekea utu uzima! (Adolescent to Adulthood)

Eneo hili limekuwa gumu karibu kwa kila mzazi walio ktk ndoa,mahusiano na linakuwa gumu zaidi kwa wazazi walitengana au kuachana.



Kwa kile nikionacho mimi ktk utafiti wangu usio rasmi sehemu kubwa ya walezi au wazazi tuameshaanza kushindwa vita hii adimu na muhimu sana kwa mustakabali wa maisha mema wa watoto wetu.

Sehemu kubwa ya wazazi walio na kipato cha juu,kati na cha chini kabisa tumefeli ktk kuwaelekeza watoto yale yalio baora ktk maisha yao! Wengi wetu tumekuwa tukijitahidi sana kutaka watoto wake ktk Tania njema Ila tumejikuta tukiishia ktk manung'uniko,mikwaruzano na migogoro mikubwa tena Mara kwa Mara na watoto hao.




Watoto Wengi wamekuwa wagumu kufuta Yale wanayoelekezwa hasa wapofikikia ktk umri huu wa miaka 14-30,na Wengi wetu tumejikuta tukikata tamaa kabisa kutokana na kuogopa majibu,kauli au vitisho watupavyo.

Wazazi na walezi wengi wamekuwa wao ndio wanawagopa watoto hata ktk kuelekeza,kuonya,kukataza, qu kuamrisha jambo Fulani ili kufanywa au kuacha kufanya na Mtoto huyo.




Kutoka na ndoa,mahusiano mengi kusambaratika,kutumia mda mwingi ktk kutafuta maisha itatufanya kushindwa kujua aina ya maisha watoto wetu wanayoishi wanapokuwa pembeni yetu.

Hatimaye nyakati za sasa kutokana na kutokuwa na ushirikiano ktk jamii,kushuka maadili tumejikuta watoto wetu wakingia ktk tabia na mambo yanayoharibu Jamii na mfumo wao wote wa maisha na kukosa maana ya yeye kuwa Mtoto au kuja ulimwenguni.




Madawa ya kulevya,ushoga,usagaji,wizi,mimba za utotoni zinazofanya kushindwa kumaliza masomo,magonjwa ya zinaa kaa ukimwi,vifo ktk umri mdogo n.k

Nimelisema hili kutokana hatua ya raisi magufuli aliyoichukua dhidi ya mwanafunzi wa kike watakaopata mimba wakiwa masomoni kuwa hawatoruhusiwa kuendelea na masomo hasa ktk kipindi hiki cha utawala wake.

Hii imetokana na mashirika na taasisi za haki za binadamu kuwa wanataka kutetea mwanafunzi wakipata mimba wakishajifungua waruhusiwe kuendelea na masomo!




Kauli hii ya maTshirika na taasisi hizi inasikitisha sana kwani hii ni sawa na sisi wazazi kuzidiwa nguvu na watoto wetu na kufuaya yale wanayojisikia wao baada ya kuona tumeshashindwa ktk kuwalea,kuwafundisha na kuwazuia jinsi ya kuepukana na mimba hizo.

Ktk hili inamaana kuwa wazazi na walezi sasa tumeshindwa vita hii na watoto wetu! Na sasa kilichobaki ni sisi wazazi kukubali na kupiga magoti kwa watoto wetu kwa kuwaacha kufanya Yale wanayoyataka wao na sio tunavyotaka sisi!!















Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "HIVI KARIBUNI WATOTO WANATARAJIA KUPORA TAJI LA USHINDI WA MALEZI TOKA VICHWANI MWA WAZAZI (WALEZI) WAO"

Back To Top