IRAN,UTURUKI ZAWAONYESHA JEURI YA FEDHA WAARABU WENZAKE,MAREKANI KWA KUPELEKA NDEGE TANO ZILIZOSHEHENI VYAKULA QATAR

Iran na Uturuki zimeamua kupeleka ndege zaidi ya tano aina ya Boeing zilizosheheni vyakula kama maziw,maji,mboga za majani,matunda na aina nyingine ili kupunguza hali ya ukosefu wa chakukla kwa taifa hilo dogo tajiri kwa gesi na mafuta duniani baada ya majirani zake kama saudi arabia,misri,bahrin,yemen na UAE kuiwekea vikwazo vya kiuchumi nchi hiyo kwa kuishutumu kuhusika na kusaidia vikundi vya kigaidi duniani.

Kila ndege moja imebeba zaidi ya tani 90 za vyakula na kufanya kuwa tani 450 za vyakula kutoka irani pekee.





Baada ya kuibuka kwa mgogoro wa ghafla wiki chache tu baada ya rais wa marekani Donald Truph kufanya ziara yake ktk mashariki ya kati kwa nchi za israel,saudi arabia na kuleta changamoto kwa nchi zote zinazoonekana kusaidi kwa kukua na kusambaa ugaidi ktk kanda hiyo na hata nje.

Baadhi ya nchi kama UAE,Misri,saudi arabia zimeamua kufuta kwa urafiki wao wa kidiplomasia,kiuchuni,kibiashara na Nchi ya Qatar kwa kuishutumu kuhusika na kusaidia wanaharakati wa Hamas,Hizbollah,serikali ya rais Asad ya syria kuendelea kufanya maangamizi kwa mashariki ya kati na duniani kwa ujumla,Mataifa haya kwa pamoja yameiwekea Qatar vikwazo vya kiuchumi ilikuacha na mipango yake hiyo kwa magaidi kama inavyoshutumiwa licha ya Qatar kupinga kauli hiyo.

Kwa mda mrefu Irani,Syria Qatar zimekuwa zikilaumiwa kwa kukumbatia magaidi na kupanga mashambulizi mbalimbali ndani na nje ya mashariki ya kati.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "IRAN,UTURUKI ZAWAONYESHA JEURI YA FEDHA WAARABU WENZAKE,MAREKANI KWA KUPELEKA NDEGE TANO ZILIZOSHEHENI VYAKULA QATAR"

Back To Top