BOSI WA ACACIA ATINGA NCHINI KUTOKA CANADA KWA NDEGE BINAFSI

Rais John pombe Magufuli jana alikuwa na ugeni wa Dharura ikulu kutoka nchini canada ambao walikuja kwa madhumuni ya kuzungumza na Rais juu ya mgogoro unaoendelea kutokota kwa zaidi ya maiezi mitatu sasa juu ya kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia ambao wanashutumiwa ktk kusafirisha makontena ya mchanga wa madini juu ya kiwango walichokubaliana,kukwepa kulipa kodi halali kwa serikali toka mwaka 1998 walipoanza kazi hiyo nchini.

Bosi huyo mr.John Thornton aliingia jana nchini kwa kutumia ndege yake binafsi kutokea nchini Canada marekani ya kaskazini ambapo kuna umbali wa kilomita 12,816 sawa na maili 7,664 kwa kutumia ndege kwa ajili ya kuja kuweka sawa maelewano juu ya mzozo huu ulitikisa hisa ktk soko la dunia,safari yake hii ilimchukua zaidi ya masaa 24 angani.






 Mr Thornton amezunguza na rais kwa kifupi na kukubaliana kuwa watafikia mwafaka vyema juu ya kuumaliza mzozo huo ikiwemo na kulipa madeni yote wanayodaiwa na serikali kama walivyokubaliana.

Acacia ni kampuni ndogo ndani ya kampuni kubwa kabisa yenye migodi sehemu mbalimnbali duniani ya Barrick Gold Mining ambapo bosi huytu anamiliki hisa za asilimia 64% ktk kampuni hii ya Acacia. ya bosi wa barrick gold mining ikiwasili jijini dar es salaam



Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "BOSI WA ACACIA ATINGA NCHINI KUTOKA CANADA KWA NDEGE BINAFSI "

Back To Top