ALIYEKUWA MGOMBEA URAIS ACT WAZALENDO BI.ANNA MGHWIRA AWA MKUU WA MKOA KILIMANJARO

Mwanamke pekee aliyeonyesh njia na uzalendo kwa wanawake wote Tanzania kwa mara ya kwanza kwa kugombea urais ktk uchaguzi mkuu wa mwak 2015 Anna Elisha Mghwira ameteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa kilimanjaro nafasi ambayo iliachwa wazi na Sadick meck sadick.

Uteuzi huu uliofanywa na Rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania Mh.John Pombe Magufuli umewafanya watu wengi kuendelea kushangaa kwa Rais kuwa na roho ya kuweza kuchaguwa watu kutoka vyama vya upinzani na kuwapa vyeo va juu kama alivyofanya kwa Agustino Liatongo Mrema kuwa mwenyekiti wa Parol,Kitila mkumbo kuwa kamishna wa Dawasco na hii ya Anna Mghwira kuwa mkuu wa mkoa kilimanjaro.

Si hivyo tu Rais magufuli amekuwa na tabia ya kuwachukua hata wakuu na walimu wa vyuo na vitengo mbalimbali na kuwapa madaraka ya juu ikiwemo ubnge wa viti maalum,kuteuliwa na hata kuwapa dhamana ya vyeo vya Uwaziri.

Taswira hii inaonyesha ni jinsi gani Rais magufuli alivyokuwa hana mambo ya ukabila,udini,uchama na hata ukanda au kungalia watun wa juu pekee.



Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "ALIYEKUWA MGOMBEA URAIS ACT WAZALENDO BI.ANNA MGHWIRA AWA MKUU WA MKOA KILIMANJARO"

Back To Top