AJABU ZA VIUMBE HAWA WATATU

Mamba uweza kukaa chini ya maji bila kuvuta pumzi kwa mda dakika 15 hadi 45 bila kuibuka na kuvuta hewa nje,ikiwa kuna kitisho cha usalama wa maisha yake au anawinda basi uweza kujizuia huko chini kwa masaa Mawili sawa na dakika 120.



Kiboko yeye ana uwezo kukaa chini ya maji kwa dakika 5 kisha uibuka na kuvuta pumzi upya,kiboko utumia zaidi ya masaa 16 kukaa ktk maji ili kupoza joto la Mawili wake!

Mwanadamu ana uwezo wa kukaa ndani ya maji kwa dakika 10-22 bila kuvuta hewa ikiwa ana Afya njema.

Kiboko dume uwa na uzito wa kilo 1600-4500 sawa na tani nne na nusu,jike kilo 1400.




Mamba uwa uzito wa kilo 1075 sawa na tani moja.

Mwadamu uwa na uzito wa kilo 50 -450.

Mamba ana nguvu kubwa za kushika na kuvuta kitu kwa kutumia meno yake hasa anapokuwa ndani ya maji zinazofikia 2125-7700 psi za presha kwa mamba wakubwa kaa wa mto Nile.




Kiboko nguvu za meno ni 1821 psi za presha wakati mwanadamu yeye ana nguvu za meno kufikia 150 psi za presha.

Tambua kuwa mamba uwinda na kula wanyama,samaki,ndege na hata wanadamu Ila hana uwezo wa kumkamata wala kumla kiboko licha kuishi na kukaa wote ktk maji.







Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "AJABU ZA VIUMBE HAWA WATATU"

Back To Top