WAKUBWA HAWA WANAIPELEKA WAPI DUNIA?

"WE CALL THEM WORLD'S SUPER POWER ALLIES"


Jamaa hawa wana uwezo wa kuvamia,kupiga,kuweka vikwazo kwa taifa lolote litakaloonekana kwenda kinyume na matakwa yao!


Wana uwezo wa kupanga jambo la uongo likaonekana kweli na kweli kuonekana uongo! (Propaganda)
Uwezo wa kuingiza au kumuondoa kiongozi yeyote wamtakae ktk taifa lolote!


Wana uwezo wa kuchonganisha watu wa taifa moja walikuwa wakiipendana wakaishia ktk uadui mkubwa!


Wana uwezo wa kujenga vituo vya kijeshi mahali popote au kusafirisha silaha nzito,kama vifaru,bunduki,ndege kwa ajili ya kupambana na mtu atakayekwenda kinyume na taratibu zao!



Wana uwezo wa kununua watu wa taifa lolote na wakafanya kazi kwa ajili yao!


Kwa kawaida wao wanapokwenda kupiga au kuvamia sehemu uuambia ulimwengu kuwa wanakwenda kuweka amani,kurudisha utu,kuondoa sheria kandamizi,ugaidi na magaidi,madikteta,kuweka haki na usawa ktk nchi hiyo Ila cha ajabu zaidi hali huwa mbaya zaidi wanapoingia mbaya zaidi wanaweza kuondoka wakaiacha nchi husika ukiwa imesambaratika Mara 1000 awali ilipokuwa hakuna haki au kutawaliwa na madikteta.

Ulimwenguni mzima unaendesha na kuongozwa kwa matakwa ya mabwana hawa ukiondoa Korea kaskazini,Cuba,China,urusi angalau ujaribu kupinga baadhi ya mambo!


Mbaya zaidi endapo mtu mmoja wa kwao atashikiliwa kama mateka au kuuwawa wako tayari kutumia nguvu kubwa na ziada ilimradi kuokoa au kulipiza kisasi kwa aliyetenda na wao wakisaha kuwa jua mamia kwa maelfu ya wanadamu wenzao ktk maeneo wanayovamia na kupiga!


Licha ya wao kujiuta wachunga haki za kibinadamu duniani la kushangaza nyumbani kwao watokako mambo magumu zaidi:-


Ubaguzi wa rangi mitaani,sehemu za kazi,ktk michezo kama mpira wa miguu,mauaji ya kiholela mitaani,ukandamizaji wa demokrasia,hakuna usawa wa jinsia,hakuna Uhuru wa kufanya utakalo,kila eneo linatawaliwa na sheria Kali,mauji mashuleni,vyuoni.


Maswali ya msingi kichwani kwangu:-


Ni kweli watu hawa wanahuruma na waafrika,Asia?


Ni kweli wanakuja kulinda amani au kutibua jamani?


Je wanapovamia eneo na kupiga je hali hubadilika na kuwa nzuri zaidi ya awali?









Si wizi wa Mali za nchi husika ndio huwaleta huku?


Ni mpaka nyakati gani dunia itaendelea kuwaangalia mabwana hawa wakifanya watakayo kwa nchi yeyote huku ikiwatazama?


Je mabwana hawa wanatengeza amani na kuwafanya watu kuwa wamoja au kusambaratisha hata utulivu mchache ukiokuwepo?


Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "WAKUBWA HAWA WANAIPELEKA WAPI DUNIA?"

Back To Top