
Wamiliki wa migodi hiyo inayofanya kazi ya kuchimba mchanga huo kwa miaka mingi wamekuwa wakikanusha kuwa wanasafirisha mchanga wenye kiwango kikubwa cha madini bali wanapeleka mchanga huo kwa ajili ya kuyeyusha madini machache tu baada ya kukosekana kwa kiwanda na mitambo ya kuyeyushia aina hiyo ya madini nchini ambayo uhitaji zaidi ya nyuzi joto 1500 na kuendelea.
Kashfa hii iliibuka baada ya Mh.Rais kutembelea bandari ya Dar es salaam ghafla na kuagiza kontena zaidi ya 20 kutosafirishwa kwenda popote pale mpaka hapo uchunguzi wa tume zaidi ya tatu alizoziunda Rais kukamilisha uchunguzi wake.

Leo ikulu saa tatu asubuhi ndion ilikuwa siku ya kukabidhiwa ripoti hiyo rasmi kwa Mh. rais na walioagizwa kufanya hivyo waliwasilisha ripoti hiyo iliyotoa uozo huo wa kilichomo ndani ya makontena ya michanga kuwa asilimia kubwa ya mchanga huo uligundulika na kukutwa na kiwango kingi cha madini ya thamni ya mabilioni ya dola za kimarekani.
Ripoti hiyo iliwaweka midomo wazi Mh Rais,waziri mkuu na makamu wa Rais wakati wakisikiliza kwa kusikia kiwango kikubwa cha mali za watanzania zilizokuwa zikipotea bila ya wao kujua.

Mda mchache baada ya tangazo hilo waziri Sospeter Muhongo amemwandikiwa Mh.Rais barua kuwa ameamua kuachia ngazi kwa cheo hiko,hata hivyo Rais na alijibu barua hiyo kwa haraka leoleo kuwa ameridhia ombi lake hilo.

Waziri Sospeter Muhongo akiwa na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh. John Pombe Magufuli

0 Comments "MUHONGO ANYOFOLEWA TENA KTK UWAZIRI WA NISHATI NA MADINI"