VIRUSI VIPYA VYA VIFAA NA MITANDAO YA MAWASILIANO VYAITESA DUNIA

Kmekuwa na mashambulizi ya mifumo na vifaa vya mawasiliano ktk nchi zaidi ya 70 duniani kote kutokana na virusi vipya vya aina ya (Ransomware) ambavyo vimeripotiwa kuingilia mifumo ya mawasiliano ktk taasisi,mashirika,makampuni,serikali,hospitali na hata ile ya kijeshi ktk nchi nyingi duniani.

Aina hii mpya ya virusi inaonekana kusumbua sana ulimwengu toka kuingizwa kwake ktk mfumo huo wa mawasiliano nchi kama mareakani,urusi na mataifa kadhaa duniani wamelalamika juu ya kushambuliwa na aina hiyo ya virusi ambavyo hupitia kwa njia ya intaneti na kuingia ktk kifaa na taarifa za mtumiaji na kuzuia kufanya kazi  na hatimaye kushindwa kuendelea na shughulia yeyote na hivyo kifaa hicho kuzima kabisa na kutowaka tena.

Urusi peke yao wameripoti zaidi ya talakilishi (kompyuta) 1,000 kuingiliwa na virusi hivyo vikali kabisa kuwahi kutokea, Baada ya kifaa chako kuathirika na virusi hivyo ujumbe wa maneno hutumwa na kukuomba kuweka kiasi cha pesa zaidi ya dola 300 kwa watu binafsi na mashirika dola 1,500 na zaidi na vyenginevyo watazima kifaa hiko na kupoteza taarifa zote za msingi.

Virusi vya mawasiliano ni aina ya programu maalum zinazotengenezwa na wataalam waliobobea kwenye maswala ya mawasiliano kwa ajili ya kuzuia,kuchukua au kupoteza taarifa fulani ktk kifaa chako cha mawasiliano kama simu,kompyuta n.k.





Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "VIRUSI VIPYA VYA VIFAA NA MITANDAO YA MAWASILIANO VYAITESA DUNIA"

Back To Top