Kumeshuhudiwa maandamano makubwa ya kila mara toka kufariki kwa kiongozi wa taifa hilo la kijamaa Bwana Hugo Chavez machi 5 2013 aliyeonekana kuiongoza nchi hiyo kwa sera zake za kibabe na kijamaa na kufanya kuwa adui mkubwa wa nchi za magharibi na marekani kutokana na misimamo yake mikali ya kisiasa.
Kwasasa nchi imekumbwa na matatizo makubwa ya ukosefu wa mafuta ya vyombo vya usafiri,chakula na huduma nyingi za msingi kutokana na sera mbovu wanazozilalamikia wananchi na kuwafanya makundi makubwa ya vijana kumw
Serikali ya Nicolas maduro imekuwa ikitumia nguvu nyingi za jeshi na polisi ktk kusitisha maandamano hayo ya makundi makubwa ya vijana yanayoambatana na uharibifu wa mali,kuchoma moto nyumba,ofisi,magari na mali nyingi za serikali.Makundi hayo ya vijana yamekuwa yakiandamana mara kwa mara ili kushinikiza kuitishwa kwa uchaguzi mkuu tena ili kuwapa nafasi wavenezuela wengi kuweza kuchagua serikali na viongozi wapya watakaoweza kulisimamia kisawawa taifa hilo la marekani ya kusini.
Zaidi ya waandamanaji 29 wamekufa na 40 wameripotiwa kuumia wiki iliyopita na kusema kushindwa kuitisha uchaguzi kwa wakati ni hali inayoashiria kuifanya ichi hiyo kuingia ktk Udikteta. Vyama vya upinzani vimekuwa mstari wa mbele kupinga mambo hayo yakiwemo ya ktaka kubadili katiba ili kumpa madaraka zaidi Maduro.
0 Comments "MIZIMU YA HUGO CHAVEZ YAMTAFUNA MADURO VENEZUELA"