
Sherehe hii inayoazimishwa kila mwaka mwezi mei imefanyika na mataifa hayo washindi kama ufaransa,marekani,uingereza na urusi kwa mbwembwe kubwa za kuonyesha gwaride mbalimbali za vikosi vya majeshi yao,silaha na mitambo mizito ya kivita.
Vita hii imegharimu roho za watu milioni 80 kwa kuuawa kwa vita,njaa na magonjwa yaliyokuwa yamekithiri kwa kipindi hiko. Sherehe hizi uhudhuriwa na wanajeshi wastaafu baadhi waliokuwepo ktk vita au uwanja wa mapambano (Veterans)

Sherehe hizi ni za kutimiza miaka 72 toka kumalizika kwa vita hiyo na kuungusha utawala huo wa WANAZI na kuachwa wasijue adolf Hitler alipo potelea mpaka hii na wengine kuamini labda alikimbilia mafachoni argentina au kujia kwa kuunguzwa moto ili usipatikane hata ushahidi. vita hii ya pili ya dunia ilipiganwa baina ya 1939-1945.
Ikumbukwe kuwa vita ya kwanza ya dunia iliyopiganwa mwaka 1914-1918 iliondoa uhai wa watu wapatao milioni 17.

0 Comments "URUSI YASHEHEREKEA USHINDI WA KUUANGUSHA UTAWALA WA WANAZI 1945"