UKWELI KUHUSU TRENI (LOCOMOTIVE)

Ilichukua nusu karne (miaka 50) kwa muingereza Richard Trevithick kutoka taifa la kwanza kuendelea kiviwanda duniani yaani Uingereza ( The great Britain) kutimiza ndoto yake ya kuunda treni ya awali inayotumia makaa ya mawe na maji ili kuzalisha mvuke (steam) utakaosukuma mashine hiyo.

Treni hii iliyofahamika kama Coalbrookdale iliyokamilika mwaka February 21/1804 na kuifanya kutimiza miaka 213 toka kuundwa kwake kufikia 2017.

Treni hii iliweza kutembea umbali wa kilomita 8.5 kwa saa moja ikiwa imebeba tani 10 za Chuma na wafanyakazi 70.

Ktk mwaka 1938 treni ziliboreshwa zaidi nakuwa na uwezo wa kusafiri umbali wa kilomita 300 kwa saa moja kwa treni za diesel na kwa sasa zipo za umeme zenye uwezo wa kusafiri umbali wa kilomita 600 kwa saa.

Treni ndio usafiri wa pili duniani kwa kubeba mizigo mizito zaidi na kwa umbali mrefu baada ya meli.

Ugunduzi huu wa treni uliisaidi sana uingereza ktk kukuza na kuendelea kiviwanda ktk miaka ya 1800s-1950.




Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "UKWELI KUHUSU TRENI (LOCOMOTIVE)"

Back To Top