TAASISI NA MASHIRIKA YA KUTETEA WANAWAKE WAHUZUNISHWA NA WABUNGE YA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONIM

Mjadala uliokuwa ukiendelea ktk bunge la jamhuri ya mungano wa Tanzania kuhusu Kuruhusu au kutoruhusu mwanafunzi wa kike kama aendelee na masomao au asiendelee pindi anapokuwa aepata ujauzito (mimba) limezua hisia kali kwa taaisisi  na wanaharakati wa haki za kibinadamu baada ya wabunge wengi kupinga swala hilo kuruhusiwa kufanyika baada ya wanafunzi wa kike kupata ujauzito kwani litachochea zaidi upatikanaji wa mimba hizo kwa kasi zaidi endapo watoto na jamii itafahamu wazi kuwa hata baada ya mimba unaweza kuendelea na masomo.

Mjadala huu unakuja baada ya idadi ya watoto wakike walio masomoni kuendelea kukosa masomo au kukatiza wakiwa katikati kwa kupata mimba au kuolewa kwa kiwango kikubwa hasa kwa nchi zetu zilizo chini ya jangwa la sahara kutokana na kukithiri kwa umasikini,kukosa elimu ya uzazi,malezi kwa watoto hawa.

Wanaharakati wa haki za kibinadamu wamesema jamii inapaswa kuelewa kuwa idadi ya wanafunzi wa kike wanaokatiza masomo kwa kupewa mimba na kuolewa ndoa za utotoni ambazo hufuta ndoto zao za maisha yao ya baadae.

Zaidi ya wasichana 27 kati ya 100 upata mimba wakiwa chini ya umri wa miaka 18

Baadhi ya ya mikoa kama ya shinyanga ndoa za utotoni ni 59%,Tabora 58%,Mara 55%,Dar es Salaam 17%

Kati ya wasichana 27 kati ya 100 uolewa chini ya umri wa miaka 18 na 36 kati ya 100 uolewa katika umri wa maika 20-24.

Tatizo hili la ndoa na mimba za utotoni limekuwa sugu hapa nchini ktk jamii kwa kuendelea kufumba macho wahalifu hawa wanaowatendea wasichana hawa matukio haya kwa kuwalinda na kutetea watu hawa na kuwaepusha na vyombo vya usalama.


Miongoni mwa mambo au sababu zinazosababisha wasichana wengi kupata ujauzito ni umbali baina ya mazingirsa wanayoishi na zilipo shule kuwa mbali zaidi hivyo kufanya kukutana na vishawishi njiani wanapokuwa wanakwenda na kurudi,suluhisho la matatizo haya ni kujenga mabweni ktk shule zote nchini inaweza kupunguza matatizo haya.

















Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "TAASISI NA MASHIRIKA YA KUTETEA WANAWAKE WAHUZUNISHWA NA WABUNGE YA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONIM "

Back To Top