
Mvua kubwa zinazoendelea nchini kwa baadhi ya mikoa kama Dar es salaam,Tanga,Kilimanjaro,Iringa,Mbeya,Kagera,Pwani na mikoa mengineyo zimeendelea kuleta madhara makubwa sana kwa miundombinu ya barabara,reli kwa kubomoa madaraja,kukata barabara zenyewe,kufanya njia nyingi kutokupitika kutokana na kuharibika kwa kuwa na tope nyingi hasa kwa zile zisizo za viwango vya lami.

Hivi karibuni eneo la barabara inayounganisha wilaya za lushoto na korogwe mkoani Tanga imekuwa haipitiki kabisa kutokana na kuporomoka kwa mawe,tope,miti na kuziba barabara hiyo,hata hivyo baadhi ya gari zimepata uharibifu wa hali ya juu kwa kuangukiwa na mawe na kufinikwa kwa tope hilo zito.
Eneo la milima ya kitonga iliyopo mkoani iringa pia kumeripotiwa kuporomoka kwa mawe na kuzuia njia hiyo na kuleta hofu kubwa kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri na hata kwa abiria wanaopita maeneo hayo hatarishi.

Hali hii inaweza kusababisha madhara makubwa endapo hazitochukuliwa hatua za dharura kwani kuna uwezekano wa mawe,tope kuja na jkuangukia magari hayo na kuuua watu waliomo ndanui,zaidi ya siku tatu sasa wasafiri wa njia ya lushoto wamenasa bila kujua nini cha kufanya kutokana na kuzibwa kwa njia hiyo muhimu.
Kwa mkoa wa Dar es salaam kumekuwa na kuzama kwa nyumba na kuharibika kwa barabara nyngi hivyo kufanya kutopitika kabisa na kufanya misongamano mikubwa ya magari njiani.
0 Comments "MVUA ZALETA GHARIKA NCHINI KWA KUKATA MAWASILIANO YA BARABARA "