
Mradi huu pindi utakapoanza na kukamilika unaonekana kuleta ahueni kubwa kwa wananchi wengi watakaopitiwa na bomba hili kubwa na wale wote wanaishi jirani na mji wa matwara mjini,Tathimini na upembuzi wa maene kama vijiji ambapo utapita ulishafanywa ikiwemo kupima na kutoa gharama zitakazotumika kulipa fidia kwa wananchi watakaochukuliwa sehemu za ardhi zao.
Hata hivyo mapaka sasa toka kufanyika kwa upembuzi huo na kukamilika bado hakuna malipo wala shughuli yeyote yalianza kufanyika kwa wananchi hata kwa mradi husika hivyo kuwaacha wana mtwara kutokuelewa wapi aua nini kimejili nyuma ya pazia na kufanya kukwama kwa mradi huo wa msingi.

Maftaa Nachuma aliendelea kulalamika zaidi kwa kusenma imefika mahali anaonekana kama tatizo kwa wananchi kwa kupata malalamiko mengi,pia amekiri kurudishwa nyuma kwa jitihada za maendeleo kwa kuafanyiwa hujuma za kushindwa kupata ushirikiano wa mda mwafaka au kunyimwa kabisa kama alivyofanyiwa ktk kunyimwa kwa gari la kuchimba visima licha ya yeye kujitolea fedha zake za mfukoni zaidi ya milioni 10.
0 Comments "MAFTAA NACHUMA AMMINYA JPM KULETA MAJI MTWARA TOKA MTO RUVUMA"