
Rais John Pombe Joseph Magufuli akiwa mkoani kilimanjaro kama mgeni rasmi ktk sherehe za kuazimisha siku ya wafanyakazi duiani kupitia shirika la kazi duniani ILO amesema amefurahishwa sana na idadi kubwa ya wananchi na wafanyakazi kwa kujitokeza kwa idadi kubwa sana ambayo hakuitegemea kabisa kwa jinsi alivyakuwa akihisi.
Magufuli alionekana kusifia mara kwa mara wafanyakzi na wananchi kwa ujumla kwa kujitokeza kwa wingi na kumpokea kwa shangwe za hali ya juu,Sherehe hizi ziliwahusisha watu na viongozi mbalimbali wa serikali,mashirika ya umma,makampuni,wafanyakazi,taasisi,mabalozi wa nchi mbalimbali, Baadhi ya viongozi hao ni Waziri mkuu mh. Majaliwa kassim Majaliwa,makamu wa rais Mh. Samia Suluhu Hassan,Spika wa Bunge mh. Jobu Ndugai,makamu spika Tuia Akson,Balazi wa china,balozi wa Ujerumani,Mkuu wa jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu bila kuasahua Mwenyeji ambae ndio mkuu wa mkoa wa kilimanjaro Mh. Said Meck Sadick na wengine wengi.

Ktk hotuba ya mh. Magufuli ktk kujibu maombi,maoni,malalamiko ya wafanyakazi wa kada mbalimbali rais alianza kusema sasa anaanza ukurasa mpya baina yake na wafanyakzi kwa kukemea swala zima la uhamisho wa wafanyakazi wengi kila wakati unaofanywa na maafisa,wakurugenzi usiofuta taratibu za msingi na haki za malipom,Rais amekemea uhamisho huo ukome na endapo itabidi kufanya hivyo basi mwajiriwa analazimika kulipwa mara moja gharama zake kabla ya kuondoka eneo husika.
Rais amegundua ubadhilifu na matumizi mabaya ya fedha na madaraka ktka eneo hilo kwa kutokuwa na lazima ya kufanya hivyo,wakati mwingine uhamisho unafanywa kwa maslahi binafsi na roho ngumu za wahudumu wa serikalio kwa nia ya kukomoa au kupata kitu kidogo.
JPM amezungumzia swala la ukaguzi na uhakiki wa wafanyakazi laki 4035000 wakiwepo hewa 16000,wafanyakaazi wenye vyeti vya kughushi 9,932,wenye vyeti vyenye utata vinatumika na mtu zaid ya mmoja 1,538,wenye vyeti vya Taaluma husika bila vyeti vya elimu 11,596 na kusema hao wote wamekuwa wakiitia hasara serikali kwa mda mrefu sana hivyo anawashughulikia kwa dhati kama alivyoanza kufukuza hao wenye vyeti vya kughushi 9,932 na kuwaambia kufikia mei 15 wawe wameondoka kwa hiyari yao vyenginevyo watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufungwa maika 7 jela.
Rais Magufuli amezungumzia na kuahidi kwa mwaka huu wa bajeti kushughulikia baadhi ya kero za wafanyakazi kama ongezeko la mwaka la mshahara,kupandisha madaraja na posho mabalimbali ambazo zilisimama toka kuingia kwake madarakani kutokana na tukio zima la uhakiki ulikua unaendeleatoka 2016.

Ombi la TUCTA la kupunguza mifuko ya hifadhi za jamii kufikia miwili tu kwani kwasasa imekuwa mingi zaidi na haina ufanisi,pia amezungumzia madeni ya wadaiwa wa bodi ya mikopo kuwa bodi toka imekopesha zaidi ya trilioni 7 toka kuanzishwa kwake na mpaka sasa imelipwa bilioni 187.4 ambapo kwasasa ilitakiwa kufikia bilioni 400 hivyo serikali imelazimika kupandisha makato ya 15%. na pia anaruusu kwa hiyari watu kulipa hadi 50% ili kumaliza madeni hayo haraka.
Pia serikali imekili kudaiwa trlioni 1.5 na mifuko ya hifadhi ya jamii toka 2010 na kulipa trilioni 1.2.5,serikali pia imekudia kuajili zaidi ya wafanyakzi 5,2000 kwa mwaka huu wa pesa na pia ameahidi kukutana na baraza la mawaziri ili kuzungumzia na kupanga zaidi juu ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi.

Ktk hali isiyokuwa ya kawaia mama mmoja jina likisomeka Amina alieonekana kubeba bango na kutaka kwenda mbele ya mh.Rais na kuzuiwa,Rais alimruhusu na kusoma bango lake lililosomeka kuwa ANADAI MIRATHI YAKE TOKA KWA MAREAHEMU MUMEWE KWA MIAKA 6 BILA MAFANIKIO Rais aliamrisha kuandiwa jina ake na namba yake ya simu ili kulisghulikia zaidi.
0 Comments "MAGUFULI ATOA MATUMAINI MAPYA KWA WAFANYAKAZI MEI MOSI KILIMANJARO "