MAFURIKO YASABABISHA BALAA KISIWA CHA SRI LANKA

Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha usiku na mchana ktk kisiwa cha sri lanka kusini mwa nchi ya India kilichopo bahari ya hindi,kisiwa hiki kinachojitegemea kama nchi kamili kimekubwa na mvua kubwa zilizosababisha mafuriko karibu eneo kubwa la nchi na kuharibu miundombinu ya barabara,reli na majengo mbalimbali zikiwemo nyumba za raia.

Mvua hizi zilizoambatana na upepo mkali,radi zinazosababisha kuanguka kwa miti na nguzo za mawasiliano,kuporomoka kwa ardhi kutoka milimani na kusababisha vifo vya watu 91 na zaidi ya 110 kupotea kusikojulikana.

Mji mkuu wa nchi hii wa Sri lanka ujulikanao kama Colombo pia umekubwa na balaa hili hivyo kuilazimu serikali kuagiza vikosi vya kijeshi kuingia mitaani na maeneo mbalimbali ya nchi ili kuhakikisha wanasaidia na kuokoa uhai wa watu walikumbwa na matatizo mbalimbali.

India imeamua kupeleka meli yake ya kijeshi ikiwa imesheheni msaada wa vyakula,madawa,nguo kwa watu walio athirika na janga hilo kubwa.

Nchi hii siku nyingi imetoka ktk mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na vikundi vya waasi wa Tamil Tiger walikuwa wakipigana na serikali kwa miaka mingi.














vijana wakisaidia watu walifukiwa ktk matope baada ya maporomoko ya ardhi kutokea.









 Daraja likiwa limefunikwa na maji na kufanya watu kukatisha kwa shida


Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MAFURIKO YASABABISHA BALAA KISIWA CHA SRI LANKA"

Back To Top