KOREA KASKAZINI WAVURUMISHA TENA BOMU USIKU WA MANANE

Taarifa mpya za siku ya jumamosi usiku korea kaskazini wamevurumisha bomu lingine kuelekea baharini na kuleta tafrani kwa majirani zake korea kusini.

Bomu hilo lenye uwezo wa kuruka umbali wa kilomita 700 sawa na maili 430 na kuruka umbali wa kwenda juu zaidi ya kilomita 2000 lililrushwa na utawala huo licha ya umoja wa mataifa,marekani,umoja wa ulaya kuiwekea vikwazo lukuki kila mara ili kuachana na mpango wake wa kutishia mataifa ya jirani na kuleta uoga kwa raia wa mataifa ya jirani.




Korea kaskazini chini ya uongozi wa kijana mdogo kim jong un aliyerithi madaraka kutoka kwa baba yake kim Jong il aliyefariki miaka ya hivi karibuni, Kijana huyu anaendeleza mbio za kijiti kutoka kwa baba yake wakiwa na ndoto ya kutengeneza bomu litakaloweza kusafiri kutoka Mji mkuu wa kwao wa pyongyang hadi bara la marekani ya kaskazini sawa na umbali wa kilomita 11048.15 ili kuweza kuipiga mareakni akiwa nyumbani kwake.



Wataalam wa mambo ya mabomu wanasema bomu hili linaaminika kuwa ni la aina mpya kabisa  kurushwa kwa jinsi ya nguvu kubwa lililokuwa nalo.

























Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "KOREA KASKAZINI WAVURUMISHA TENA BOMU USIKU WA MANANE"

Back To Top