EMMANUEL MACRON KUKABIDHIWA KIJITI CHA URAISI KUIONGOZA UFARANSA LEO

Kijana mdogo kabisa kuwahi kuiongoza ufaransa Emmanuel Macron aliyezaliwa 21/12/1977 kwasasa akiwa na umri wa miaka 39 tu ndiye rais mdogo kabisa anayekwenda kukabidhiwa kijiti cha kuiongoza ufaransa leo hii na mwenyeji wake Rais Francois hollande aliyeiongoza ufaransa toka mwaka 2012-2017.

Emmaneul Macron kabla ya kuchaguliwa kuwa rais wa ufaransa kwa kupigiwa kura kwa 65.5% ya kura zote alishashika nyadhifa nyingi ndani ya serikali ya rais anaeondoka madarakani leo kama kuwa Waziri wa fedha,viwanda nsa uchumi.
Macron kupitia cha chake cha En Marche! alishinda kwa kishindo kikubwa zaidi kuliko marais waliokuwepo kabla yake kama Jacques Chirac 1995-2007,Nicolaus Sarkozy 2007-2012 na Francoiz hollande 2012-2017 ambapo Macron anakabidhiwa kijiti hiko cha kuiongoza Ufaransa ikiwa ni miongoni ma mataifa tajiri na yenye uchumi wa juu ulaya na hata duniani kwa ujumla,Ufaransa imeendelea zaidi ktk viwanda.

Ufaransa iliwahi kutawala zaidi ya mataifa 29 duniani na 21 kati ya hayo yanatoka barani afrika na yanazungumza lugha ya kifaransa kama lugha yao kuu ya Taifa.

Macron anaapishwa ktk jumba la rais kongwe lililopo ktk jiji la Paris lijulikanalo kama Elysee linalotumika kama makazi na ofisi ya rais toka 1848,jengo hili limeanza ujenzi wake 1718.









Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "EMMANUEL MACRON KUKABIDHIWA KIJITI CHA URAISI KUIONGOZA UFARANSA LEO"

Back To Top