JAPAN YAPITISHA MSWADA WA KUMRUHUSU MFALME WA HIMAYA HIYO KUJIUZULU

Japan ni miongoni mwa nchi chache duniani zenye kuendelea kuongozwa kwa mfumo wa kifalme (Monarchy) na serikali kuongozwa zaidi na waziri mkuu kuliko mfalme au malkia ambaye yeye mara nyingi ni mtu wa kukaa na kupata heshima ya juu zaidi pamoja na kizazi chake chote.

Uingereza,uholanzi pia ni miongoni mwa nchi zenye kuongozwa kwa mtindo huo wa himaya za kifalme,Wafalme na malikia wa nchi hizi uendelea kuongoza nchi kwa kurithishana kizazi baada ya kizazi na mtu uendelea kuongoza hadi pale atakapokufa.

Japan wameamua kuweka sheria ya kumuwezesha kiongozi wao huyo wa tabaka la juu kabisa endapo kama atahitaji kujiuzulu kutokana na mambo mbalimbali ikiwemo umri mkubwa,magonjwa ya mda mrefu kuweza kujiuzulu yeye mwenyewe.

Mfalme wa japan Bw. Akihito alyezaliwa Desemba 23 1933 kwasasa ana umri wa miaka 83 akiwa ni mfalme wa 125 ktk himaya hiyo ya kijapan na kuiongoza nchi hiyo toka januari 7 1989 hadi sasa,kwasasa anaonekana umri wake ni mkubwa na kusumbuliwa kiafya mara kw mara hivyo kumlazimu kutaka kujiuzulu, akihito alioa mkewe anayeitwa Michiko  Shoda mnamo 1959.

Japan ni miongoni ya mataifa yalioendelea zaidi ktk viwanda,sayansi na teknologia ya hali ya juu ikiwa na uchumi wa juu kabisa,wasomi wengi na miji iliyopangiliwa vyema.

Japan maarufu kwa kutoa magari Toyota,pikipiki za honda na vifaa vya aina nyingi vya umeme.

Mtendaji mkuu wa shughuli za serikali ni waziri mkuu ambae kwasasa anaitwa Shinzo Abe,Serikali hii ya japan inafanya kazi zake ktk mji mkuu wa Tokyo.




















Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "JAPAN YAPITISHA MSWADA WA KUMRUHUSU MFALME WA HIMAYA HIYO KUJIUZULU"

Back To Top