HATIMAYE CHINA YAJITENGENEZEA NDEGE KUBWA YA ABIRIA KWA KUTUMIA WATAALAM WA NDANI


Siku ya ijumaa mei 5 2017 shirika la kutengeneza ndege la Commercial Aircraft Cooperation of China (COMAC) wamefanikisha ndoto kubwa ya taifa la china kujitengenezea ndege zake zenyewe za abiria ambayo walikuwa wakiiota kwa nguvu zote toka 1972 kwa kuanzishwa kwa shirika hilo la serikali.

Comac wamefanikiwa kurusha ndege yao ya COMC C919 kwa mda wa dakika 90 angani na kutua salama ktk uwanja wa ndege wa Pudong ulioko Shanghai China,Ndege hii yenye kubwa sawa na ndege za Boeing 737 na Airbus 320,yenye uwezo wa kubeba abiri 168 na kuruka umbali usiopungua kilomita 5,555 kwa kutembea kilomita 300 kwa saa moja.

Ndege hii ya Comc C919 imewavutia wateja wakubwa duniani na tayari mashirika mbalimbali ya usafiri wa anga wameshaagiza zaidi ya ndege 570 za aina hii kutoka kwa makampuni 23.

Ndoto ya china ya kujitengenezea ndege yake yenyewe ilikuwepo toka Pale Rais wa Marekani alipotembelea kiwanda cha ndege cha Boeing 707 kilichopo china.

Rais wa china wa sasa Bwana XI JI PING amewambia wachina waache tabia ya kuona kununua vitu kutojka nje ni rahisi zaidi kuliko kujitengenezea wenyewe ndani.



Shirika la Comac tayari limeshatengeneza ndege 6 za majaribio maalum.


















Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "HATIMAYE CHINA YAJITENGENEZEA NDEGE KUBWA YA ABIRIA KWA KUTUMIA WATAALAM WA NDANI"

Back To Top