
Baada ya kukamatwa kwa Joaquim Guzman (El- Chapo) ambae alionekana kuisumbua sana serikali ya mexico kwa mda mrefu zaidi ktk kuongoza genge la uharifu na uuzaji wa madwa ya kuleya nchini humo na marekani la SINALOA sasa jeshi la mexico limtia nguvuni kiongozi au bosi mkuu wa genge hilo la uhalifu anaejulikana kama Damaso Lopez Nunez.

Watuhumiwa hawa wote wawili watapelekwa ktk vyombo vya sheria vya marekani ili kushtakiwa kwa makosa wanayoyafanya ndani ya taifa hilo kiasi cha kutishia uhusiano baina ya nchi mbili hizi kwa kutaka kujengwa kwa ukuta mkubwa na mrefu zaidi ya kilomita 3000 ili kukomesha biashara hiyo haramu inayoshamiri ndani ya marekani na kuharibu kizazi cha vijana wengi.
Magenge haya yanayojihusisha na shughuli hizi za uuzaji,usambazaji wa madawa ya kulevya si mageni kwani yalikuwepo toka miaka 1970s na kusumbua sana nchi za italia,marekani,mexico,panama,colombia na brazili.

Makundi haya pia ujihusisha na mauaji,uuzaji wa binadamu,uteseji,utekaji nyara na mashambulizi ya visasi.
0 Comments "BOSI WA GENGE LENYE NGUVU LA MADAWA YA KULEVYA AKAMATWA MEXICO"