35 WAFARIKI KTK AJALI MBAYA YA GARI WAKIWA SAFARINI ARUSHA


Mwanafunzi wapatao 35 wamefariki baada ya Gari baina ya Costa kupoteza muelekeo kutokana na mvua Kali iliyokuwa inanyesha aneo hili pamoja na ugeni wa Dereva wa Gari hiyo Mali ya Shule ya Lucky Vincent iliyopo jijini Arusha eneo la  kwa Mrombo.






Ajali hiyo iliyotokea majira ya saa tatu asubuhi ktk bonde la  mto Mrera takribani kilomita 150 kutoka arusha Mjini na kilomita 25 kuelekea geti la hifadhi ya taifa  ya ngorongoro pia ikiwa  ilisalia kilomita 5 tu kufika ktk sehemu ya shule Tumaini English medium juniors walipokuwa wanaelekea kufanya mitihani wa mazoezi ya kujipima kama ilivyokuwa kawaida yao.

watu hao wakiwemo wanafunzi 32 wavulana 13 na wasichana 20,walimu 2 na madereva 2 walifariki papo hapo mda mfupi baada ya ajali hiyo mbaya kabisa,Rais Magufuli ametuma salam za rambirambi kwa ndegu na jamaa wa marehemu,Rais wa kenya Uhuru Kenyata naye amemtumia salam za pole Rais Magufuli kwa msiba huo mkubwa.





Gari hiyo iliyokosea njia na kuingia ktk korongo kubwa na kufanya kuharibika vibaya sehemu za mbele na kusababisha vifo vya wanafunzi hao papo hapo kutokana na mstuko na kugongana wao kwa wao na vitu vya Gari.



Ajali ikitokea majira ya saa  tatu asubuhi hii leo jumamosi  mei 6 2017.





























Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "35 WAFARIKI KTK AJALI MBAYA YA GARI WAKIWA SAFARINI ARUSHA"

Back To Top