WATUMISHI ELFU TISA (9000) VYETI FEKI KUNYOLEWA VIPARA NA JPM APRIL 30 2017

Rais John Pombe Joseph Magufuli jana akiwa ktk uzinduzi wa Majengo ya hosteli mpya za chuo kikuu cha Dar es salaam amewapa salamu watumishi wote wa serikali ktk ngazi mbalimbali kama Afya,elimu,wakuu wa mikoa,wilaya na idara nyeti za serikali atawashughulikia kisawasawa pindi ripoti kamili itakapomfikia mikononi mwake.

Zoezi hili la uhakiki wa taarifa mbalimbali na vyeti vya elimu za watumishi wote wa serikali ulianza mapema toka Rais Magufuli alipoinia madarakani baada ya serikali kugundua kuna idadi kubwa ya wafanyakazi kuliko uhalisia,watu wanatmia nyaraka sizizo halali ikiwemo vyeti feki,kutumia vyeti vya watu wengine,kuwepo kwa wafanyakazi hewa lakini wanalipwa mishahara na stahiki zao zote,wafanyakazi walioacha kazi au kufariki lakini bado wanalipwa mishahara pia.

Kiasi hiki cha ubadhilifu wa pesa na mali za umma ulimlazimisha JPM kuunda timu ya wataalam na kupita kuhakiki nyaraka na taarifa zote za wafanyakazi ili kabaidi ukweli na kufanikiwa kugundua zaidi ya watumish hewa 17,000.

Mwishoni mwa mwezi huu april 30 Rais anatarajia kupokea ripoti kamili ya wafanyakazi walio na taarifa na nyaraka za vyeti feki za elimu. Rais ameahidi kuwashughulikia bila kuangalia nani au ana cheo gani.


Share :

Facebook Twitter Google+ Lintasme

Related Post:

0 Comments "WATUMISHI ELFU TISA (9000) VYETI FEKI KUNYOLEWA VIPARA NA JPM APRIL 30 2017"

Back To Top