Simu ni kifaa cha umeme kinachotumika kwa ajili ya kuwasiliana baina ya watu wawili au zaidi walio maeneo tofauti au mbalimbali,umbali wao kati yao watu wawili uwafanya washindwe kuwasiliana ana kwa ana.
Simu zipo za mkononi na zile za awali za kuunganishwa kwa waya ndio kutoka sehemu moja hadi nyingine,nikiwa na maana ya (Mobile phones and land line) simu za ardhini ndio simu za kwanza kugunduliwa na kuanza kutumika toka mwaka 1876.
Leo nitazama kidogo ktk simu zetu za mkononi(mobile or handset) ambazo ndio nyingi zaidi na utumika nawatu wengi zaidi duniani kwa sasa.
Simu hizi za mkononi zilianza kutmika rasmi mnamo april 3 1973 pale bwana Martin Cooper raia wa canada alipofanikiwa kutengeneza simu ya mkononi kupitia kampuni ya kimarekani ya Motorola ya Dyna TAC 8000x ikiwa kama jina la simu hiyo.
Simu hii ya Dyna TAC 8000x ilikuwa na uzito wa kilo 2,betri yake ina uwezo wa kukaa na chagi kwa masaa 8,na kuchagiwa kwa saa 10 ili kujaa kabisa,pia ilikuwa na uwezo wa kuongea kwa dakika 30 mfululizo bila kuisha kwa chagi yake,lakini ilikuwa nina uwezo wa kuhifadhi namba za simu na majina yake 30 tu.
Kwa mara ya kwanza simu hii iliuza zaidi ya simu 300,000 laki tatu duniani kote kwa bei ya dola za kimareakani $3,995 sawa na shilingi za kitanzania 8389500 milioni nane laki tatu themanini na tisa elfu na mia tano kwa simu moja tu.
Simu hii ya Dyna TAC 8000x ndio ilikuwa simu ya kwanza kutambuliwa na kukubalika na mamlaka ya shirika la viwango la vifaa vya umeme na mawasiliano la FCC federal communication comission mwaka 1973
Mnamo mwaka 1979 japan ndio lilikuwa taifa la kwanza kwa kuwa na simu na mitandao iliyoenea nchi nzima ikifuatiwa na denmark,sweden,norway na finland ktk miaka ya 1981.
Hata hivyo mitandao na simu ziliendelea kuboreshwa na kuongezwa matumizi zaidi kadri siku zinavyosogea hadi sasa tuko ktk mifumo ya kisasa kama Android,window phone n.k,kwa upande wa mitandao hasa mtandao buibui (internet) ilitoka ktk 0G 1973,2G 1983,3G 1993 na mwaka 2012 kuingia ktk 4G.
Simu hutumika kwa mawasiliano kwa njia mbalimbali zikiwemo kuongea,ujumbe wa maneno,picha na video. kwsasa simu zimekuwa ni bei rahisi sana kiasi hadi kununuliwa kwa dola 10 tu sawa na elfu ishirini tu 20000.
Kwasasa simu ni miongoni mwaka kifaa cha muhimu sana kiasi watu wengi wanamiliki ili kurahisisha mawasiliano na kufanya mambo ya kibiashara,kiuchuni na kijamii kuwa mepesi kabisa.
0 Comments "SIMU YA MKONONI:MACHACHE USIYOYAFAHAMU KUHUSU SIMU YAKO (HAND OR MOBILE PHONE) "