
Hichgi ndicho kilichomkuta mwalimu Dyness mkuu wa shule ya msingi Kigonzile iliyoko mkoani iringa baada ya vyombo vya habari vinavyomilikiwa na Sahara media (radio free,kiss fm,startv) vyenye makao makuu mkoani Mwanza baada ya kumtembelea shuleni kwake hapo na kumuhoji juu ya mzaingira mabovu na chakavu yalioko shuleni hapo kiasi cha kutishia usalama wa walimu na wanafunzi wenyewe.
Sehemu kubwa ya majengo ya ofisi na madarasa ya shule hiyo yamechakaa paa zake na kuta zake nyingi zimeweka nyufa kubwa kiasi cha kuhisi siku na nyakati yeyote ile kuta zinaweza kuanguka na kuleta madhara kwa watoto au walimu.

Mkuu wa shule hiyo alipohojiwa alizungumza ukweli kuwa shule hiyo imechakaa sana na wao pamoja na wanafunzi wanaishi ktk mazingira magumu na hatarishi ktk kzi yao kiasi hata wanafunzi hawavutiwi na hali hiyo mbaya,kumbe hilo la kutoa taarifa likawa kosa kwake.
Siku chache baada ya habri hiyo kurushwa SShirika la bima la taifa NIC walitembelea shuleni hapo kwa kujionea mazingira halisi n kutoa msaada w mifuko 135 ya saruji ili kupunguza tatizo hilo na kukuta mkuu huyo wa shule ameshavuliwa madaraka hayo na kuwa mwalimu wa kawaida ktk shule hiyohiyo.
Wadu wa elimu na mbunge wa jimbo hilo Bi Kabati wamelaani kitendo hicho na kuahidi watakisimamia hadi haki ipatikane kwani hali hii inarudisha nyuma bidii kwa walimu wengi kwani wao wanafanya kazi ktk mzaingira magumu sana

0 Comments "MKUU WA SHULE AVULIWA MADARAKA KWA KUZUNGUMZA UKWELI KUHUSU MAZINGIRA CHAKAVU YA SHULE YAKE"