RAIS MAGUFULI KUWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA RELI YA KISASA PUGU

Rais John Pombe Magufuli leo yuko mji wa Pugu pembeni kidogo mwa jiji la Dar es salaam kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi kama ishira ya kuzindua rasmi kwa ujenzi wa Reli ya kiwango cha kati kama ilivyokuwa ahadi yake.

Shughuli hii ya uzinduzi imehudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh.Paul Makonda pia mabalozi wa uturuki,ureno na ujerumani wao wakiwa ndio nchi zitakazotoa makandarasi watakaojenga  reli hiyo ya treni ya umeme.

Ujenzi huu wa reli hii utachukua zaidi ya miezi 30 sawa na miaka miwili na miezi nusu kwa kipande cha kilomita 300 kutoka Dar es salaam hadi morogor,kampuni kutoka ujerumani,ureno na uturuki ndio wamechaguliwa ktk dhabuni hii ya ujenzi,kutakuwa na stesheni 6 kubwa.

Treni hii itakuwa na uwezo wa kutoka Dar-morogoro kwa masaa matatu,Dar-Dodoma masaa 7,Dar-Mwanza Kwa saa 10 tu na itatembea mwendo wa kilomita 160 kwa saa moja.

Gaharama za maradi huu hadi kwisha utagharimu zaidi pesa za kimareakni dola bilioni mia moja na mbili milioni mia tisa tisini (1,029,900,000 na ukiongeza kodi ya serikali dola 185,382,000 jumla ya gharama kamili ni dola za kimarekani 1,215,282,00.

Kutoka Dar-Morogoro kilomita 300, Morogoro-Makotpora 336,Makutopora-Tabora 294,tabora-isaka 133 kilomita na Isaka hadi Mwanza ni kilomita 248 sawa na jumla ya kilomita 1,311 kutoka Dar es salaam hadi Mwanza.

Reli hii itasaidia kuapatikana kwa ajira wakati wa ujenzi na hata baada ya kukamilika kwake,kusafirisha mizigo mingi na mizito kwa haraka,kuboresha utalii nchini hivyo kukuza uchuni kwa kasi huku ikiokoa Barabara zisiharibike kwa haraka kwa kubeba mizigo mizito.



Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "RAIS MAGUFULI KUWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA RELI YA KISASA PUGU"

Back To Top