GAVANA WA BENKI KUU (BOT) BENNO NDULU: RIPOTI YA BENKI YA DUNIA YAITAJA TANZANIA NCHI INAYOKUWA KWA KASI KIUCHUMI

Gavana wa benki kuu ya Tanzania Bw.Benno Ndulu amevieleza vyomo vya habari kuwa hali ya uchumi wa nchi iko imara na inazidi kukua kwa kasi ya 7% kwa mwaka ktk kila nyanja,makusanyo ya mapato kwa mwaka yameongezeka kwa kiasi kikubwa baada ya kuzuia mianya ya upotevu wa mapato mengi ya serikali kwa njia ya ukwepaji kodi,rushwa na uwajibikaji duni kwa watendaji wa serikali.

Kwasasa kumekuwa na matumizi makubwa ya kutuma na kutoa pesa kwa njia za mitandao ya simu na kufanya kuingiza pesa nyingi,kuboreshwa kwa miundombimu,mawasiliano n.k

Benki ya dunia ambayo hivi karibuni imeikopesha tanzania pesa nyingi ili kushughulikia miradi mbalimbali nchini na kuahidi kulipa kwa riba ndogo ya 5% tu kwa mkopo huo.

Aidha gavana aliendelea kusema watu wote wanaolalamika kuwa hali ya uchumi imekuwa mbaya kwao ni wale wote waliozea kupata pesa chafu kwa njia ya rushwa,wizi,utapeli,ufisadi na ubadhilifu wa pesa za umma, kwakuwa sasa serikali imezuia  mianya hiyo ya u[potevu wa pesa kwa kiwango kikubwa na kufanya waliozoea hali hiyo kulalamika hovyo, Benno aliongeza kuwa watu wote watakao fanya kazi halali watapata pesa kama kawaida.


Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "GAVANA WA BENKI KUU (BOT) BENNO NDULU: RIPOTI YA BENKI YA DUNIA YAITAJA TANZANIA NCHI INAYOKUWA KWA KASI KIUCHUMI"

Back To Top