
Haikuishia hapo bali nchi za magharibi ziliona ni bora kuuangusha utawala huo kabisa ili kuondoa dhulma kwa wairaki wenye dini ya kishia na wakurdi wachache waliokua wakiuawa na kunyanyaswa na utawala huo ikiwemo na kutowaweka ktk ngazi za ungozi za utawala wa BAATH kama chama Tawala.
Kweli mkakati huo ulifanikiwa na kuuangusha utawala huo wa mabavu na hatimaye kufikia Desemba 30 2006 Aliyekuwa Rais wa Iraq Bw. Saddam Hussein mzaliwa wa Tikrit alihukumiwa kifo cha kunyongwa na mahakama za ndani kwa makosa ya uhalifun wa kivita na mauaji ya watu wengi.
Sasa ni miaka 10 toka kunyongwa kwa kiongozi huyo aliyeonekana kuwa dhalimu kwa wairaki wachache imepita.

Swali la kujiuliza nini kilichobakia kwa wairaki kushindwa kutulia na kujenga taifa lao ikiwa Mtawala waliomwita diktekta amshafariki miaka mingi iliyopita?
Sasa tunasikia mara washia,wakurdi,wasuni mara islamic state(IS) kuwa wao kwa wao ndio wanapambana kuwania madaraka ambayo kwa sasa asilimia 80 wanamiliki washia.
Hivi leo machi 25 2017 kumeripotiwa kuuawa zaidi ya watu 200 huko mji wa Mosul kutokana na mashambulizi ya ndege za kivita za marekani na washirika wake wakiwa wanawasaka waasi wa IS ambao wanaaminika kuwepo na kujificha ndani ya majumba ya watu.
Hali ya iraq imejitokeza huko libya,syria,yemen,afaghanstan na misri.
Swali la msingi la kujiuliza: Je tatizo lilikuwa uongozi au kiongozi? au matatizo yapo kwa watu wanaoongozwa?

Mbona nchi zimeharibika na kuendelea kuharibika zaidi ya zilivyokuwa nyakati za watawala hao madhalimu?
Mbona maisha ya watu wa mataifa hayo wamekuwa kama ndege wasio na mama zao kwa kutangatanga na njaa,kukosa makazi,elimu,kukimbia nchi,kubakwa na kukiukwa kwa haki za kibinadamu zaidi ya nyakati za tawala za viongozi hao madhalimu?
Mimi na wewe hatujui kipi bora baina ya zamani na sasa? ila nina imani watu syria,iraq,Congo DRC,iraq,afghanstan,yemen na kwengineko wanajua zaidi baina ya ubora wa zamani na sasa!

0 Comments "SADDAM HUSSEIN AMENYOGWA 2006:NINI KILICHOBAKIA NYUMA KWA WAIRAKI KUENDELEA KUUWANA"