Rubani wa shirika la usafiri la kimarekani (American airline) Bw.William Grubbs maarafu kama Mike amefariki mda mfupi tu baada ya kutoka uwanja wa ndege wa Albuqueue jiji jimbo la New Mexico siku ya jumatano mchana.
Ndege hiyo aina ya Boeing 737 yenye namba za usajili 1353 ilifanikiwa kushuka tena uwanja wa ndege huo ikiwa salama.
Sababu za kifo cha rubani huyo hazikuwekwa wazi kwani ilikuwa ghafla na wala hakuripotiwa kuumwa kabla ya kuanza safari yake.
Kumekuwa na historia ya marubani Wengi kufa wakiwa angani ktk kazi zao hizo kama ilivyotokea mwaka 2015.
0 Comments "RUBANI WA SHIRIKA LA USAFIRI WA ANGA LA MAREKANI AFARIKI AKIWA ANGANI"